Gambo awapiga dongo wapinzani, asema kama hawatabadilika watapotea
Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo amefunguka na kusema kuwa wapinzani wa Tanzania kama hawatabadili aina ya siasa wanazozifanya sasa basi watapotea kwani serikali ya awamu ya tano imepata Rais ambaye hataniwi na wala hatishiki.
Gambo amesema kuwa wapinzani badala ya kuanza kupiga porojo zisizo na msingi, wajipange tu kumsaidia Rais John Pombe Magufuli ili aweze kutekeleza mambo aliyoahidi kwa Watanzania kwa miaka mitano.
"Nataka niwaambie wanasiasa hawa wa upinzani wasipobadilisha aina ya siasa wanayofanya kwa ninavyoiona mimi serikali ya awamu ya tano watapotea, kwa sababu tumepata Rais ambaye hatanii.
"Unajua wameshazoea wengine wakitishwa tishwa kidogo wanaingia mitini huyu Magufuli akinyooka amenyooka, ananyoosha rula tu utaamua mwenyewe ukae kushoto au kulia.
"Kwa hiyo mimi niwashauri tu itakuwa vizuri badala ya kupiga porojo wajipange kumsaidia Rais aweze kutekeleza mambo aliyoahidi kwa Watanzania kwa miaka mitano" alisema Gambo
Mbali na hilo Mkuu wa Mkoa huyo wa Arusha amesema kuwa kwa mtu yoyote ambaye ataonekana kutaka kuikwamishan serikali basi watadili naye asubuhi, mchana na jioni.
"Kwa mtu yoyote ambaye ataonekana kuikwamisha serikali isitekeleze malengo yake nataka niwahakikishie kwa uwepo wangu hapa tutahangaika naye asubuhi, mchana na usiku kwa mbinu zote zile.
"Kama wanataka porojo wasubiri 2020, sasa hivi kama wanataka tusaidiane kupeleka huduma na maendeleo kwa watu, haiwezekani tukawa na serikali au nchi ambayo kila siku ni porojo tu, kila siku siasa"alisisitiza Mrisho Gambo
Taarifa muhimu kwa Wakurugenzi wa Halmashauri zote nchini Toka Wizara ya Afya
Taarifa muhimu kwa Wakurugenzi wa Halmashauri zote nchini Toka Wizara ya Afya
Tarehe 22 June 2017, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania alilipia VIUADUDU vya kutokomeza Mbu wa Malaria lita 100,000 na kuagiza vigawanywe kwenye Halmashauri zote nchini.
Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Mhe Ummy Mwalimu anapenda kuwatanganzia Wakurugenzi wa Halmashauri zote nchini kuwa VIUADUDU hivi vitaanza kugawiwa leo (jana) kwa Halmashauri za Mikoa 14 yenye kiwango kikubwa cha Maambukizi ya Ugonjwa wa Malaria.
Mikoa hii (na kiwango cha maambukizi ya malaria kimeonyeshwa kwenye mabano) ni;- Kagera (41%), Geita (38%), Kigoma (38%), Ruvuma (23%), Tabora (20%), Mtwara (20%), Mara (19%), Morogoro (14%), Shinyanga (17%), Lindi (17%), Pwani (15%), Mwanza (15%), Katavi (14%) na Simiyu (13%),
Mikoa mingine ambayo haijatajwa itagawia Viuadudu katika Awamu ijayo.
Idadi ya Lita zitakazogawanywa kwa kila Halmashauri zilizo katika Mikoa hii tayari imeshaainishwa.
Wizara inawakumbusha Waganga Wakuu wa Mikoa/Wilaya kufanya Upuliziaji wa Viuadudu kwa kuzingatia Miongozo ya Wizara ya Afya. Hii itawezesha kupata matokeo tarajiwa ya kutokomeza mbu ili kudhibiti ugonjwa wa Malaria nchini.
Aidha, Wizara ya Afya inapenda kumshukuru kwa dhati na kumpongeza Mhe.Rais Dkt. Magufuli kwa kuongeza chachu katika Mapambano dhidi ya Malaria Nchini.
Imetolewa na;
Catherine Sungura
Kaimu Msemaji- Idara Kuu Afya
26 June 2017
Mwinyi Atabani Rais Magufuli Awe Rais wa KUDUMU Milele wa Tanzania
Mwinyi Atabani Rais Magufuli Awe Rais wa KUDUMU Milele wa Tanzania
Rais Mstaafu Ali Hassan Mwinyi amesema kama si matakwa ya Katiba ya nchi, uongozi wa Rais John Magufuli ulipaswa kuendelea kuwapo miaka yote.
Alisema laiti ingelikuwa Katiba iliyopo haikufupisha muda wa uongozi wa rais, angeshauri Rais Dk Magufuli awe Rais wa Tanzania wa siku zote.
Alikuwa akizungumza katika Viwanja vya Mnazi Mmoja Dar es Salaam jana, alipokuwa akitoa salamu za Eid El Fitri.
Mzee Mwinyi alisema mambo anayoyafanya Rais Dk Magufuli ni mazuri na yanalipeleka Taifa mbele.
Hii ni mara ya pili kwa kiongozi huyo kutamka hadharani namna anavyokunwa na utawala wa sasa wa Rais Magufuli.
Mwinyi alisema Magufuli ameweza kufanya mambo mengi mazuri kwa kipindi kifupi kuliko yaliyowahi kufanywa na watangulizi wake akiwamo yeye (Mwinyi).
Katika kauli yake ya jana, Mzee Mwinyi alisema Rais Magufuli amefanikiwa kulipeleka Taifa mahali pazuri na amerejesha nidhamu katika maeneo mbalimbali ya kazi nchini.
“Nchi imetulia, leo mnakwenda madukani, hospitali, ofisini unapata huduma nzuri.
“Hayo ndiyo tuliyoyataka, kupata Serikali itakayokuwa na watumishi ambao watawatumikia watu na hivyo ndivyo inavyofanyika sasa kwa sababu tumempata kiongozi tuliyenaye leo (Rais Magufuli),” alisema na kuongeza:
“Huyu kiongozi ni wa kumuenzi sana, ni wa kumsaidia sana, ni wa kumsifu sana… si kumsifu kwa uongo, uongo, ni kumsifu kwa kazi nzuri anayoifanya si kwa manufaa yake bali kwa manufaa ya Watanzania wote pamoja na mimi niliyesimama hapa.
“Raia anataka nini tena baada ya haya? Analindwa, anashughulikiwa, anayoyataka raia ndiyo anayoyataka Rais wetu… lakini kwa kuwa tuna Katiba basi twende na Katiba yetu.
“Husia wangu kwenu Watanzania wote, tumtii na kumsaidia Rais wetu ili mambo yaende vizuri kama yalivyo sasa. Wazee wanasema hivi. ‘kidole kimoja hakivunji chawa’. Tumsaidie ili mambo yaende hivi kama yanavyokwenda”.
Akizungumzia alipokutana na Rais Dk. Magufuli Ikulu baada ya mwaka mmoja wa uongozi wake, alisema yako baadhi ya maeneo ambayo aliyafanya kwa mafanikio makubwa ikilinganishwa na wakati uliopita.
Aliyataja baadhi ya maeneo hayo kuwa ni mapambano dhidi ya rushwa akisema hatua zilizochukuliwa katika mwaka mmoja zimedhihirisha kasi kubwa ya kukabiliana na tatizo hilo ikilinganishwa na wakati uliopita.
“Rushwa ilikuwapo tangu enzi ya Hayati Mwalimu Nyerere … aliipondaponda kabisa lakini hakuimaliza, na sote tuliosalia ni hivyo hivyo, kila mmoja amefanya kwa kiasi chake, lakini Rais Magufuli kwa mwaka mmoja ameleta ‘surnami’, nafurahi sana,” alisema Alhaji Mwinyi.
Eneo jingine ni kuimarisha utendaji kazi Serikalini akisema hatua zilizochukuliwa na Serikali ya sasa zimeongeza kasi.
Aliwataka viongozi na wananchi kuunga mkono juhudi hizo.
“Tuliobaki tumsaidie, tumsaidie kwa kumuombea dua, tumsaidie kurekebisha kwa kusema ukweli pale ambako watu wanapotosha.
“Tusiwaache watu wakapata nafasi ya kuongea uongo, kila mtu anaweza kuwa anasema kutokana na nia yake na lengo lake, lakini hakuna asiyejua kuwa kazi aliyoifanya mwenzetu ni nzuri nzuri, nzuri ya ajabu,” alisisitiza.
Lowassa Mikononi mwa Polisi Leo........Ni Kufuatia Wito wa DCI Aliyemtaka Afike Polisi saa Nne
Lowassa Mikononi mwa Polisi Leo........Ni Kufuatia Wito wa DCI Aliyemtaka Afike Polisi saa Nne
Aliyekuwa Waziri Mkuu wa Tanzania, Edward Lowassa ametakiwa kuripoti katika Ofisi ya Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI) leo saa nne asubuhi.
Lowassa ambaye ni Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) amepewa wito huo kwa njia ya barau bila kuelezwa sababu za yeye kutakiwa kufanya hivyo.
Msemaji wa CHADEMA, Tumaini Makene na Lowassa mwenyewe wote wamethibitisha kupata taarifa za wito huo huku wakisema si chama wala mhusika anayejua sababu za kuitwa.
Aidha, katika mahojiano aliyofanya Lowassa na The Citizen kwa njia ya simu, amesema kuwa anadhani kuitwa kwake kuna uhusiano na kauli aliyoitoa mwishoni wa juma wakati wa futari kuhusu Masheikh wa Uamsho.
Lowassa alimtaka Rais Magufuli kuingilia kati suala hilo ambapo Masheikh kadhaa wanashikiliwa kwa zaidi ya miaka minne sasa bila maendeleo yoyote ya tuhuma zinazowakabili. Masheikh hao ambao walikamatwa Zanzibar wanatuhumiwa kwa ugaidi ambapo Lowassa alitaka Rais aingilie kati ili kesi hiyo iweze kusikilizwa.
“Sina hakika kama hii ndio sababu, lakini nahisi tu. Ila ukweli utafahamika nitakapokutana na DCI,” alisema Lowassa kwenye mahojiano hayo ya simu.