SORRY MADAM -Sehemu ya 19 & 20 (Destination of my enemies)

SORRY MADAM -Sehemu ya 19 & 20 (Destination of my enemies)

MWANDISHI: EDDAZARIA G.MSULWA
ILIPOISHIA
 Eddy akajikuta akitetemeka kwa hasira na uchungu mwingi. Machozi yakazifi kumwagika, huku akiwa ameyang’ata meno yake kwa hasira kali. Taratibu damu za pua zikaanza kumwagika, kizunguzungu kikali kikamkata, akayumba mara ya kwanza ya pili walinzi wake wakamdaka asianguka chini.

Tukio hilo likamuogopesha sana Shamsa, aliye simama nyuma yake, kwa mara nyingine nguvu zikamuishia Shamsa na kujikuta akikaa chini mwenyewe bila hata kupenda. Roho ya Rahab, ikazidi kumuuma kwani uwezo wa kutenda msaada kwa familia ya Eddy, anao ila akifanya msaada wa kuwafufua, watu wote watamkimbia, na kuamini kwamba yeye si mwanadamu na itakuwa ni miongoni mwa kasfa chafu kwa raisi Praygod, kwamba ameoa jinni.
  
ENDELEA
Madaktari waliopo katika eneo hilo wakaanza kumpatia Eddy huduma ya kwanza pamoja na Shamsa, ikawalazimu kuweza kusimamisha hudmua za mazishi kwa muda, kusubiria wahusika wakuu kkukaa katika hali nzuri. Baada ya lisaa, Eddy na Shamsa wakarejea katika viwanja vya hapo kwenye jumba lake kuendelea na mazishi ya familia yake. Rahab hakuwa na jinsi zaidi ya kuacha mazishi hayo kuweza kufanyika, huku moyoni mwake akizidi kuumia, akimuhurumia kijana mdogo Junio, kwani umri unampasa sana kuweza kuendelea kuishi katika dunia hii.

Viongozi wakubwa wakaanza kuondoka katika jumba la Eddy, kila mmoja akiamini kwamba kazi ya Mungu haina makosa na wengine wakiingiwa na hofu pamoja na mashaka makubwa ya kutaka kujua ni lini Mzee Godwin anaweza kukamatwa mikononi mwao.

“Eddy jikaze kaka yangu, tutazidi kuwa pamoja”
Rahab alizungumza maneno ya kumfariji Eddy huku akiwa amemkumbatia
“Sawa dada Rahab”
“Ina bidi upae mapumziko ya kwenda mbali na hapa, ili akili yako ikatulie”
“Hapana Rahab, hapa ni nyumbani kwamngu na ndipo walipo lala wapenzi wangu, siwezi kwenda popote nitakaa hapa hapa”
“Hapana Eddy, inabidi ukatafute sehemu ya kwenda kutuliza akili wewe pamoja na Shamsa, tambua ya kwamba unavyo endelea kukaa na kutazama hayo makaburi huo weza kusahau kamwe”

“Ni kweli siwezi kusahau, ila……”
Eddy akastukia akipigwa busu zito la mdomo na Rahab, jambo lililo mstua sana.
“Madam samahani unafanya nini?”
Eddy alizungumza huku akijitoa mikononi mwa Rahab
“Unaogopa nini Eddy, tambua hapa tupo chumbani peke yetu”
“Namuheshimu muheshimiwa”
“Hayupo”
Rahab alizungumza huku akianza kuvua kitenge alicho jifunga kiunoni mwake na kubakiwa na skintait, pamoja na tisheti nyeusi alivyo vaa, iliyo bandikwa picha ya Junio, Phidaya pamoja na mama Eddy.
                                                                                                ***
Mapigo ya moyo ya Mzee Godwin yakaanza kumuenda mbio, akajaribu kumtingisha Manka aweze kuamka, ila Manka hakuweza kujibu kitu chochote zaidi ya kuendelea kukaa kimya. Mzee Godwin gafla akasikia minong’ono ya watu nyuma yake, akageuka na kukuta vijana wawili wakiwa wamesimama huku wakichukua tukio la kuwaka moto la gari hiyo ndogo.
Walipo muona mzee Godwin wakastuka, kwani nao ni miongoni mwa watu walio weza kuiona picha yam zee Godwin kwenye mitandano ya kijamii akitafutwa kama Rubin na jeshi la polisi la Tanzania.
“Huyu si ndio yule gaidi”

Mmoja aliropoka huku akiigeuzia simu yake upande aliopo mzee Godwin ili kumchukua video. Kama mbogo aliye uliwa mwanaye, mzee Godwin akanyanyuka kwa kasi ya ajabu na kuwarukia vijana hao masharo baro. Akaanza kuwatandika ngumi za kutosha huku akiwatukana matusi ya uchungu sana. Vijana hao walilia kama watoto wadogo, wakajutia ni kwanini walisimamisha gari na kuja kushuhudia ajali hiyo. Mzee Godwin akachomoa mkanda wa suruali yake na kuandelea kuwachapa vijana hao kwa hasira kali, hadi wakapoteza fahamu.
Mzee Godwin akamgeukia Manka, kwa bahati nzuri akamkuta akitingisha tingisha mkono mmoja, kwa haraka akamuweka begani na kuanza kukimbia naye kuelekea alipo simamisha gari la polisi, akamuingiza Manka ndani na kuondoka naye katika eneo hilo,

Kila alipo mtazama binti yake huyo, waliye potezana naye miaka mingi ya nyuma roho yake ikaingiwa na furaa kubwa sana, moyoni mwake akaanza kumuomba Mungu ampe binti yake nafasi nyingine ya kuweza kuishi.
Majira ya saa mbili usiku akafika katika     handaki alilo muacha Tom, kwa haraka akafungua mfuniko wa kuingilia kwenye handaki hilo kisha akamshusha Manka ambaye bado fahamu hazijamrejea.

“Tom fungua mlango wa chumba cha kwanza”
Mzee Godwin alimuamrisha Tom huku akiwa anahema sana kutokana na kuchoka sana pmoja na wasiwasi mwingi unao mtawala. Akamlaza Manka juu ya kitanda.
“Babu huyu naye ni nani?”
“Utamjua hembu tumpe nafasi ya kuweza kupumzika?”
“Amefanyaje?”
“Heiii Tom sihitaji maswali Mengi”
Mzee Godwin alizungumza kwa hasira na kutoka nje ya chuma hicho, Toma akamtazama kidogogo Manka usoni kisha na yeye akatoka.
                                                                                                 ***
Wasamaria wema walo kuwa wakikatika katika barabara kuu, yakutokea mikoa ya Tanga na Arusha, wakasimama kwenye sehemu walipo ona moshi mwingi ukiendelea kuonekana katika upande wa pili wa barabara. Abiria waliomo katika basi la Ngorika, wakashuka kwenda kujaribu kuangalia gari hilo linalo teketea kwa moto.

Wakakuta vijana wawili wakiwa wamelala pembeni huku wakionekana kupoteza fahamu na miili yao ikiwa imajaa makovu ambayo, hakuna ambaye aliweza kuyatilia mashaka kwani waliamini kwamba ajali hiyo ya gari ndogo ndio imeweza kusababisha majeraha hayo.
“Niwazima hawa?”
Jamaa mmoja alizungumza huku akiwatazama. Kijana mwengine mrefu na mweusi kiasi, akawatazama vijana hao jinsi walivyo lala chini, baadhi ya watu wakataka kuwanyanyua.

“Hembu musiwanyanyue mara moja, sogeeni pembeni”
Alizungumza na kuwafanya watu wengine kumshangaa, kwani majeruhi hao wanahitaji msaada wao na si kuwaacha katika eneo hilo.
“Wewe kijana mjinga kweli, hao wangekuwa ni wadogo zako ungewaacha waendelee kulala hapo chini?”
Mzee mmoja wa kichaga alimjia juu kijana huyo anaye onekena ni mstaarabu na mtulivu sana, mwenye sura ya kipole.
“Mzee wangu nimewaomba na sijataka kutimia nguvu, hivi munavyo ona hawa wamepata ajali kweli?”

“Wewe unaonaje?”
Mzee huyo aliendelea kumropokea kijana huyo, aliye achia tabasamua pana kisha akaendelea kutazama sehemu walipo lala vijana hao. Kila alipo zidi kuchunguza kwa umakini eneo hilo, ndipo alipo gundua kwamba kuna mtu ambaye aliweza kuwadhuru vijana hao kwa kuweza kuwapiga sana.

Kitu kilicho zidi kumshangaza kwa vijana hao, shawakuweza kuporwa kitu cha aina yoyote, simu zao zipo katika eneo la tukio. Akachukua simu za vijana hao wawili, kwa bhati nzuri moja ya simu bado ilikuwa inaendelea kurekodi tukio katika eneo hilo. Akaisave video hiyo kisha akaanza kuitazama, sauti za vijana hao zikasikika kwenye video hiyo huku picha ya gari hilo linalo malizikia kuteketea kwa moto.

Video hiyo ikamuonyesha mzee Godwin, akiwa amemshikila binti mmoja, ila gafla mshika kamera ya simu hiyo, akastukia akiangushwa chini na kuanza kulia kwa uchungu mkali ikiashiria kwamba mzee huyo aliweza kuwapiga vikali.
“Haya munaweza kuwachukua vijana hao”
Kijana huyo alizungumza huku akizichukua simu hizo, kisha akaituma video hiyo kwenye simu yake kisha akaituma makao makuu alipo kuwa ameitwa kwa ajili ya kazi maalumu
                                                                                                            ***
     Agnes na Jaquline baada ya kufanya tukio la kuituma video ya vitisho kwa bwana Rusev, wakaagana na mzee ambaye aliweza kuwafundisha mbinu nyingi za kupambana kutumia miili yao pasipo kutumia silaha za moto.

Agnes aliweza kufuzu kwa asilimia mia, katika kujua mbinu hizo za kupambana. Moja kwa moja wakafunga safari hadi mjini Mosscow, huku wakiwa wameziweka nywele zao katika mfumo ambao si rahisi sana kwa watu kuweza kumstukia Agnes kwamba ni muuaji aliye weza kuhusika na kifo cha waziri wa mambo ya nje wa Marekani bwana Paul Henry Jr, mwaka mmoja ulio pita.
Share:

No comments:

Post a Comment

Categories

Ordered List

  1. Lorem ipsum dolor sit amet, consectetuer adipiscing elit.
  2. Aliquam tincidunt mauris eu risus.
  3. Vestibulum auctor dapibus neque.

Sample Text

Lorem ipsum dolor sit amet, consectetur adipisicing elit, sed do eiusmod tempor incididunt ut labore et dolore magna aliqua. Ut enim ad minim veniam, quis nostrud exercitation test link ullamco laboris nisi ut aliquip ex ea commodo consequat.

Definition List

Definition list
Consectetur adipisicing elit, sed do eiusmod tempor incididunt ut labore et dolore magna aliqua.
Lorem ipsum dolor sit amet
Consectetur adipisicing elit, sed do eiusmod tempor incididunt ut labore et dolore magna aliqua.

Support

Need our help to upload or customize this blogger template? Contact me with details about the theme customization you need.

Pages