kikutwa wamesimama na wanafunzi wa kike, viboko 12
Uongozi wa kata ya Nyehunge wilayani Sengerema umepitisha sheria ya kuwacharaza viboko 12 au faini ya Sh10,000 wanaume watakaokutwa wamesimama na wanafunzi wa kike.
Sheria hiyo ndogo imepitishwa juzi kwenye kikao cha maendeleo ya kata (WODC) baada ya tatizo la wanafunzi kukatisha masomo kutokana na kupata uja uzito kuzidi kuwa sugu.
Ofisa mtendaji wa Kata ya Nyehunge, Mabula Enock alisema sheria hiyo itasaidia kudhibiti vitendo vya wanaume wanaoshawishi wasichana kufanya nao mapenzi na baadaye kuwapa ujauzito unaokatisha ndoto zao.
“Tumelazimika kupitisha sheria hiyo ili kuungana na mkuu wa wilaya yetu, Emmanuel Kipole aliyeagiza wanaume watakaokutwa wamesimama na wanafunzi wacharazwe viboko au kutozwa faini ya Sh10, 000 ama vyote kwa pamoja,” alisema Enock.
Agizo la mkuu huyo wa wilaya alilitoa Oktoba mwaka 2017 wakati akikaribisha wanafunzi 81 kujiunga na masomo ya kidato cha tano katika Shule ya Sekondari ya Nyehunge.
Diwani wa kata hiyo, Charles Mbogo alisema kitendo cha kukatiza masomo si cha kuungwa mkono, hivyo adhabu inapaswa kuongezwa na kuitaka jamii kuachana na suala hilo.
Kwa mujibu wa takwimu zilizotolewa na ofisa elimu ya sekondari wa Buchosa, Benjamini Siperato halmashauri hiyo ina jumla ya wanafunzi 1,136 katika shule 20 za sekondari 20 na mwaka 2016/17 wanafunzi 18 wa kike walipata ujauzito, hivyo jamii inapaswa kuacha tabia ya kuwarubuni watoto wa kike.
No comments:
Post a Comment