Mwijage azindua kiwanda cha kwanza cha mita za luku Dar
Mwijage azindua kiwanda cha kwanza cha mita za luku Dar
Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Charles Mwijage amezindua kiwanda cha Inhemeter ambacho kitakuwa kinazalisha mita za luku na kuziuza kwa mashirika ya ugavi wa umeme nchini.
Kiwanda hicho ambacho ni cha kwanza kujengwa hapa nchini na cha nne Afrika kina soko la uhakika la kuuza mita 500,000 kwa mwaka kwa Shirika la Umeme nchini (Tanesco), Wakala wa Umeme Vijijini (Rea) na Shirika la Umeme Zanzibar (Zeco).
Mwijage aliyataka mashirika hayo kutumia fursa ya kuwepo kwa kiwanda hicho kuboresha huduma zao huku akisisitiza kwamba kitakuwa na manufaa mengi ikiwemo ajira kwa vijana 100 na mashirika kutotumia fedha za kigeni kuagiza mita nje ya nchi.
“Ninamuomba mwekezaji kuzalisha bidhaa nyingi zenye ubora wa kimataifa na bei nafuu sokoni,” alisema Mwijage wakati akizindua kiwanda hicho jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki.
Alisema Serikali ya Awamu ya Tano imedhamiria kujenga uchumi wa kati na viwanda ifikapo 2025 na kuzinduliwa kwa kiwanda cha Inhemeter ni uthibitisho kuwa azma hiyo imeshaanza kutekelezwa kwa vitendo.
“Tunahitaji viwanda vitakavyo mpunguzia gharama mlaji au mtuamijia pamoja na kuzalisha ajira kwa vijana wetu,” alisema huku akitaka aliye tayari kuanzisha kiwanda ofisi yake iko wazi kumsaidia.
Waziri Mwijage alimpongeza mwekezaji huyo kwa uamuzi wake wa kuja Tanzania.
“Wakati umefika wa kuondokana na uchuuzi. Tunataka tuzalishe wenyewe hapa nchini na tuuze nje, simaanishi kuwa hatuhitaji bidhaa za nje, zije zile tu zenye ubora stahili,” alisema.
Pia alisema anayo furaha kushuhudia uzinduzi wa kiwanda kipya cha 3,307 katika kipindi kifupi.
Awali, akizungumza kwenye hafla hiyo, Mshauri Mkuu wa kiwanda hicho ambaye pia ni katibu mkuu mstaafu wa Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Dk Adelhem Meru alivishauri vitengo vya manunuzi nchini kusaidia ujenzi wa viwanda.
“Ningependa kutoa wito kwa vitengo vya manunuzi kuunga mkono kwa dhati azma hii ya Serikali ya Awamu ya Tano ya kujenga uchumi wa kati na viwanda. Ninafahamu vitengo hivi vina nafasi nzuri sana,” alisema.
Kwa upande wake, Mkurugenzi Mtendaji wa kiwanda hicho, Abraham Rajakili alisema Inhemeter ni kampuni yenye uzoefu wa miaka 20 katika tafiti, uzalishaji na usambazaji wa mita za luku na tayari wameshasambaza katika zaidi ya nchini 60 dunia.
“Kiwanda hiki kitakuwa na uwezo wa kuzalisha mita za luku milioni moja kwa mwaka na pia kuajiri mafundi mia moja Watanzania,” alisema.
PICHA: Sugu amefika Mahakamani tayari kusikiliza Hukumu ya Kesi yake
PICHA: Sugu amefika Mahakamani tayari kusikiliza Hukumu ya Kesi yake
Ulinzi umeimarishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Mbeya ambako itatolewa hukumu ya kesi inayomkabili mbunge wa Mbeya Mjini, Joseph Mbilinyi maarufu Sugu na Katibu wa Chadema Kanda ya Nyanda za Juu Kusini, Emmanuel Masonga.
Katika eneo la mahakama wapo askari wa Kikosi cha Kutuliza Ghasia (FFU) wakiimarisha ulinzi nje ya jengo. Tayari washtakiwa wameshafika mahakamani.
Mahakama leo Februari 26,2018 inatoa hukumu ya kesi ambayo Sugu na Masonga wanashtakiwa kwa kosa la kutumia lugha ya fedheha dhidi ya Rais John Magufuli.
Wawili hao wanadaiwa kutenda kosa hilo kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika Desemba 30,2017 eneo la Uwanja wa Shule ya Msingi Mwenge jijini Mbeya.
Hukumu inatarajiwa kutolewa na Hakimu Mkazi Mfawidhi, Michael Mteite aliyesikiliza kesi hiyo. Upande wa mashtaka na wa utetezi ulikamilisha ushahidi Februari 9,2018.
Jamhuri iliwasilisha mashahidi watano na kielelezo kimoja cha sauti iliyodaiwa kurekodiwa na shahidi wa tano, Inspekta Joram Magova.
Upande wa utetezi uliwasilisha mashahidi sita wakiwamo Sugu na Masonga waliokana kutamka maneno wanayoshtakiwa kuyatoa.
Washtakiwa walitetewa na mawakili Sabina Yongo, Boniface Mwabukusi na Hekima Mwasipu kabla ya kujitoa, hivyo sasa wanawakilishwa na Peter Kibatala.
Kwa mara ya kwanza, Sugu na Masonga walifikishwa mahakamani Januari 16 na kusomewa mashtaka na Wakili wa Serikali Mkuu, Joseph Pande aliyeeleza upelelezi ulikuwa umekamilika na walikuwa tayari kuendelea na usikilizaji
Nassari afikishwa mahakamani Arumeru
Nassari afikishwa mahakamani Arumeru
Mbunge
wa Arumeru Mashariki (Chadema), Joshua Nassari amefikishwa katika
Mahakama ya Wilaya ya Arumeru akisubiri kusomewa shitaka linalomkabili.
Nasari
amesema jana alikwenda Kituo cha Polisi Usa River kufuatilia silaha
yake iliyochukuliwa na askari wakati wa uchaguzi wa Serikali za Mitaa
mwaka 2014.
Nassari amesema alipofika polisi alielezwa kuwa ana kesi ya kumshambulia mtendaji kosa analodaiwa kutenda mwaka 2014 .
Sheki Mfinanga ambaye ni wakili wa Nassari amesema hajui mteja wake anakabiliwa na shtaka gani.
"Jana walisema alishambulia lakini hatujui leo anashitakiwa kwa kosa gani ndiyo tunasubiri," amesema.
Dk Slaa: Sijaja Tanzania kuapishwa kuwa balozi
Dk Slaa: Sijaja Tanzania kuapishwa kuwa balozi
Balozi mteule, Dk Willibrod Slaa amesema amekuja nchini kwa ajili ya kushughulikia usajili wa Hospitali ya CCBRT.
Katibu
mkuu huyo wa zamani wa Chadema, ametoa kauli hiyo leo Februari 6, 2018
wakati akihojiwa katika kipindi cha 360 kinachorushwa na Kituo cha
Televisheni ya Clouds.
“Familia
yangu nimeiacha Canada, wengine wanajua, sikuja kwa sababu ya ubalozi.
Mimi ni mwenyekiti wa CCBRT ndicho kimenileta na wengine mnafahamu
katika nchi yetu mengi yanafanyika,” amesema.
Novemba
23 mwaka jana, Rais John Magufuli alimteua Dk Slaa kuwa balozi, lakini
mpaka sasa hajaapishwa na kupangiwa kituo cha kazi.
Dk
Slaa ambaye kwa sasa anaishi Canada alitangaza kuachana na siasa
kutokana na kutofautiana na chama chake katika kumpokea Edward Lowassa
aliyehama kutoka CCM na baadaye kupitishwa kuwa mgombea urais kupitia
muungano wa Ukawa.
Alisema chama chake hakikutekeleza makubaliano waliyoafikiana ya kuwapokea baadhi ya makada wa CCM akiwamo Lowassa.
Januari
29, 2018, Dk Slaa alikutana na kufanya mazungumzo na Rais Magufuli,
Ikulu Dar es Salaam na kumshukuru kwa kumteua kuwa Balozi na kuahidi
kuwa yupo tayari kutekeleza majukumu atakayopangiwa kwa kutanguliza
maslahi ya Taifa.
Katika
kipindi hicho, Dk Slaa ameulizwa kama amekuja kula kiapo na kupangiwa
kituo cha kazi, lakini amepinga jambo hilo na kubainisha kuwa amekuja
kushughulikia usajili wa hospitali hiyo kwa kuwa yeye ni mwenyekiti wa
bodi.
Amesema kwa mujibu wa mabadiliko ya sheria, CCBRT inatakiwa kujiandikisha upya vinginevyo itafutwa.
Kuhusu
taarifa kuwa ameajiriwa katika duka kubwa la bidhaa za nyumbani
(Supermarket) la Costco lililopo Oakville, Toronto nchini Canada,
amesema: “Hizo ni propanganda nisingependa kuzizungumza lakini
Supermarket inayozungumzwa si kama mnavyofikiri ni kubwa.
“Kitu
kikubwa tunatofautiana katika mtazamo, fikra tunavyofanya vitu vyetu.
Canada haina mwenyewe kuna raia wa kutoka kila nchi. Sisi hapa tunasema
hapa kazi tu lakini kule ni maisha. Unakuta waziri anatoka ofisini kwake
anakwenda kufanya kazi nyingine, baadaye anatoka na kwenda kufanya
nyingine. Kufanya kazi tatu ni kawaida.”
Ametolea
mfano ufanyaji kazi wa Canada na Tanzania amesema baadhi ya Watanzania
huingia ofisini na kusoma magazeti, au kutumia simu kufanya biashara
zao.
“Canada
utaingia ofisini na simu au ipad lakini utaiacha getini na matokeo yake
nchi ile ni matajiri. Watu ni matajiri kila mtu ana utambuliso wa
maisha mazuri ni kwa sababu wanafanya kazi na huduma zote ziko vizuri,”
amesema.
Kuhusu
kufunga ndoa amesema: “Siasa za Tanzania zilichangia mimi kutokufunga
ndoa kwa kipindi chote lakini Februari 2016 kule Canada nilifunga ndoa
(na Josephine Mushumbusi), ile si ndoa kwani tulishakaa, kanisa
ilichokuja kufanya ni kuhalalisha tu.”
CHADEMA Yapata Pigo Tena....Ni Baada ya Mgombea Wake Kuhamia CCM Siku Tatu Baada ya Kuzindua Kampeni
CHADEMA Yapata Pigo Tena....Ni Baada ya Mgombea Wake Kuhamia CCM Siku Tatu Baada ya Kuzindua Kampeni
Chadema
kimepata pigo baada ya mgombea wake wa udiwani Kata ya Manzase wilayani
Chamwino Mkoa wa Dodoma, Mashaka Chalo kujiunga na CCM pamoja na
wanachama wengine 131.
Chalo
amehama Chadema siku ya tatu tangu chama hicho kikuu cha upinzani
nchini kuzindua kampeni katika Kata hiyo na kunadiwa jukwaani na mbunge
wa viti maalum, Kunti Majala.
Uchaguzi
wa ubunge jimbo la Siha, Kinondoni na katika Kata 10 nchini utafanyika
Februari 17, 2018. Uchaguzi katika Kata hiyo unafanyika baada ya
aliyekuwa diwani, Peter Madanya (CCM), kufariki dunia mwishoni mwa mwaka
jana.
Mgombea
huyo amehamia CCM Februari 4, 2018 katika kijiji cha Manzase wakati wa
uzinduzi wa kampeni za chama hicho na kupokewa na Naibu Katibu Mkuu wa
CCM (Bara), Rodrick Mpogolo.
Mbunge wa Mtera (CCM), Livingstone Lusinde amesema uamuzi wa Chalo kujiuzulu ni ushindi kwa chama tawala.
“Mpogolo
unaweza kufungua kampeni hizi na kisha kuzifunga maana kazi imekwisha.
Tulikuwa na wagombea watatu, lakini kuondoka kwa huyu, CCM tunaona
kazi imekwisha. Wagombea wengine waliobaki hata tukilala usingizi
hakuna kitu ushindi ni wetu,” amesema.
Mgombea wa CCM katika Kata hiyo ni Amosi Mloha.
Lusinde amesema Chadema walimpitisha Chalo dakika za mwisho kuwania udiwani bila kujua kuwa alikuwa pandikizi la CCM.
Akizungumza katika mkutano huo Chalo amesema amerejea CCM kwa sababu ni chama chake na kimemlea.
Mahakama yaagiza Nabii Titto apime upya akili
Mahakama yaagiza Nabii Titto apime upya akili
MAHAKAMA
ya Wilaya ya Dodoma imeagiza mkazi wa mtaa wa Ng’ong’ona Manispaa ya
Dodoma Tito Machibya, maarufu kama ‘Nabii Tito’ (45) kupimwa akili upya
katika Taasisi ya Afya ya Akili ya Mirembe Isanga mkoani Dodoma ili
kujiridhisha kama ana matatizo ya akili.
Licha
ya kuagizwa mtuhumiwa huyo kufanyiwa vipimo upya, mahakama pia imetaka
kuwasilishwa kwa vielelezo kama kweli ana tatizo hilo kama alivyoieleza
mahakama.
Nabii Tito anashtakiwa kwa kosa la kujaribu kujiua kwa kutumia wembe.
Hakimu
Mkazi Mfawidhi wa Mahakama hiyo, James Karayemaha, alisema jana kuwa
kutokana na mshtakiwa kuieleza mahakama kuwa ana matatizo ya akili na
alifanya tukio hilo kutokana na kusikia vitu ambavyo vilikuwa
vinamwamuru akate, mahakama itabidi ipate vielelezo ambavyo
vitathibitisha anachokisema.
Karayemaha
alisema kutokana na kifungu namba 219 (2) cha Sheria ya Mwenendo wa
Mashauri ya Jinai, kama mshtakiwa atabainika kweli ana matatizo ya afya
ya akili, mahakama itaamua kuwa alivyofanya tukio hilo hakuwa na akili
timamu, hivyo hana hatia.
“Mshitakiwa
anadai kuwa ana matatizo ya akili na amekuwa akitibiwa katika hospitali
mbalimbli ikiwemo ya Maweni. Mahakama hii inaagiza vielelezo vyake
vyote viletwe hapa lakini pia apelekwe kwenda kufanyiwa uchunguzi wa
afya ya akili Mirembe Isanga,” alisema Karayemaha.
Pia
alisema kama mshtakiwa atabainika kuwa hana tatizo lolote la afya ya
akili kwa mujibu wa vielelezo vyake pamoja na vipimo atakavyofanyiwa,
atakuwa na kesi ya kujibu.
“Kutokana
na hili aliloiambia mahakama kuwa ana matatizo ya akili hata suala la
dhamana tunaliweka pembeni kwanza kwa sababu hawezi kujieleza lakini
kama itabainika kuwa hana matatizo ya akili kutokana na vielelezo
vitakavyoletwa pamoja na vipimo vitakavyofanyika, suala la dhamana
litafanyiwa kazi,"alisema.
Hata hivyo alisema mshtakiwa huyo anarudi rumande hadi kesi hiyo itakapotajwa Februari 19, mwaka huu.
Wakati kesi itakapotajwa vielelezo vyote pamoja na vipimo vinatakiwa kuwa tayari vimeshawasilishwa mbele ya mahakama hiyo.
Nabii Tito anashtakiwa kwa tuhuma za kutaka kujiua kwa kujikata
Bombardier Nyingine na Boeing 787 Kutua Nchini Julai Mwaka Huu
Bombardier Nyingine na Boeing 787 Kutua Nchini Julai Mwaka Huu
Ndege
mbili; moja aina ya Bombardier na nyingine kubwa Boeing 787 yenye uwezo
wa kubeba abiria 262 zilizonunuliwa na serikali, zinatarajiwa kuwasili
nchini Julai mwaka huu.
Serikali
imenunua ndege hizo ikiwa ni mkakati wa kuimarisha Shirika la Ndege
(ATCL) ili limudu ushindani kwenye biashara ya kusafirisha abiria na
kujiendesha kwa faida.
Akiwasilisha
taarifa ya shughuli za Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu kwa
kipindi cha Januari 2017 hadi, jana, mjini hapa, Mwenyekiti wa kamati
hiyo, Prof. Norman Sigalla, alisema wamejulishwa kuwa pamoja na ndege
mbili mpya aina ya Dash 8 Q400, Julai serikali inategemea kupokea ndege
zingine mbili ambapo moja ni Dash 8 Q400 na nyingine aina ya Boeing 787
yenye uwezo wa kubeba abiria 262.
Alisema
kwa sasa ATCL ina ndege tatu zinazofanya safari ndani na nje ya nchi,
lakini akasisitiza kuwa biashara ya ndege inahitaji mikakati mikubwa ya
kibiashara kuweza kuingia katika soko la ushindani.
"ATCL
iangaliwe kama kampuni ya kibiashara na siyo kutoa huduma na ijitangaze
kwenye vyombo rasmi vya kimataifa ambavyo huonyesha safari za ndege
duniani," alisema.
"Kampuni
ijipange kuingia katika soko kwa kujitangaza kwenye vyombo vya habari,
majarida, vipeperushi, kujali wateja, kuwa na bei nafuu ili kuhakikisha
abiria wengi wanatumia ndege hizo."
Prof.
Sigalla pia alisema Mamlaka ya Viwanja vya Ndege (TAA) inashauriwa
kuhakikisha viwanja vya ndege visivyokuwa na hati vinapimwa kisha
kupatiwa hati miliki.
Alisema viwanja hivyo pia vinapaswa kuwekewa uzio kuepusha uvamizi wa maeneo jambo ambalo huleta migogoro na wananchi.
"Ili
kuongeza udhibiti na ulinzi katika viwanja vya ndege vilivyopo mipakani
kama vile Mtwara, Kigoma na Kagera kuepusha viwanja hivyo kupitishwa
biashara haramu," alisema.
Maofisa wa Jumuiya ya Ulaya (EU) Wamtembelea Tundu Lissu Kumjulia Hali
Maofisa wa Jumuiya ya Ulaya (EU) Wamtembelea Tundu Lissu Kumjulia Hali
Maofisa
watatu wa Jumuiya ya Ulaya (EU) jana Februari 5,2018 wamemtembelea
Mbunge wa Singida Mashariki (Chadema), Tundu Lissu anayeendelea na
matibabu nchini Ubelgiji.
Lissu
alishambuliwa kwa zaidi ya risasi 30, Septemba 7 mwaka jana na
kupelekwa Hospitali ya Rufaa ya Dodoma na siku hiyohiyo alihamishiwa
Hospitali ya Nairobi alilazwa hadi Januari 6,2018 alipohamishiwa
Ubelgiji katika Hospitali ya Chuo Kikuu cha Leuven, anakoendelea na
matibabu.
Katika
taarifa yake kwa vyombo vya habari aliyoitoa jana Februari 5,2018 Lissu
amewataja maofisa hao kuwa ni Mkuu wa Idara ya Pembe ya Afrika na
Afrika Mashariki katika Wizara ya Nje ya EU, Patrick Simonnet.
Wengine
ni Mkuu wa Dawati la Tanzania katika EU, Marta Szilagyi, Vania
Bonalbert ambaye ni ofisa wa ubalozi wa EU Tanzania anayeshughulikia
masuala ya utawala bora na haki za binadamu na Hortensia May Lyatuu.
Amesema ujumbe wa maofisa hao mbali ya kumjulia hali walifanya mazungumzo ya masuala mbali mbali yanayohusu Tanzania.