CHADEMA Yapata Pigo Tena....Ni Baada ya Mgombea Wake Kuhamia CCM Siku Tatu Baada ya Kuzindua Kampeni

CHADEMA Yapata Pigo Tena....Ni Baada ya Mgombea Wake Kuhamia CCM Siku Tatu Baada ya Kuzindua Kampeni

Chadema kimepata pigo baada ya mgombea wake wa udiwani Kata ya Manzase wilayani Chamwino Mkoa wa Dodoma, Mashaka Chalo kujiunga na CCM pamoja na wanachama wengine 131.

Chalo amehama Chadema siku ya tatu tangu chama hicho kikuu cha upinzani nchini kuzindua kampeni katika Kata hiyo na kunadiwa jukwaani na mbunge wa viti maalum, Kunti Majala.

Uchaguzi wa ubunge jimbo la Siha, Kinondoni na katika Kata 10 nchini utafanyika Februari 17, 2018. Uchaguzi katika Kata hiyo unafanyika baada ya aliyekuwa diwani, Peter Madanya (CCM), kufariki dunia mwishoni mwa mwaka jana.

Mgombea huyo amehamia CCM  Februari 4, 2018 katika kijiji cha Manzase wakati wa uzinduzi wa kampeni za chama hicho na kupokewa na Naibu Katibu Mkuu wa CCM (Bara), Rodrick Mpogolo.

Mbunge wa Mtera (CCM),  Livingstone Lusinde amesema uamuzi wa Chalo kujiuzulu ni ushindi kwa chama tawala.

“Mpogolo unaweza kufungua kampeni hizi na kisha kuzifunga maana kazi imekwisha. Tulikuwa na  wagombea watatu, lakini kuondoka kwa huyu,  CCM tunaona kazi imekwisha. Wagombea wengine waliobaki  hata tukilala usingizi hakuna kitu ushindi ni wetu,” amesema.

Mgombea wa CCM katika Kata hiyo ni Amosi Mloha.

Lusinde amesema Chadema walimpitisha Chalo dakika za mwisho kuwania udiwani bila kujua kuwa alikuwa pandikizi la CCM.

Akizungumza katika mkutano huo Chalo amesema amerejea CCM kwa sababu ni chama chake na kimemlea.
Share:

No comments:

Post a Comment

Categories

Ordered List

  1. Lorem ipsum dolor sit amet, consectetuer adipiscing elit.
  2. Aliquam tincidunt mauris eu risus.
  3. Vestibulum auctor dapibus neque.

Sample Text

Lorem ipsum dolor sit amet, consectetur adipisicing elit, sed do eiusmod tempor incididunt ut labore et dolore magna aliqua. Ut enim ad minim veniam, quis nostrud exercitation test link ullamco laboris nisi ut aliquip ex ea commodo consequat.

Definition List

Definition list
Consectetur adipisicing elit, sed do eiusmod tempor incididunt ut labore et dolore magna aliqua.
Lorem ipsum dolor sit amet
Consectetur adipisicing elit, sed do eiusmod tempor incididunt ut labore et dolore magna aliqua.

Support

Need our help to upload or customize this blogger template? Contact me with details about the theme customization you need.

Pages