Waziri Wa Afya Atoa ONYO Kwa Wanaosambaza Picha za Waliofariki Ajali ya MV Nyerere
Waziri wa Afya maendeleo ya Jamii jinsia Wazee na Watoto Ummy Mwalimu ameonya usambazaji wa picha miili ya ajali ya Mv-Nyerere iliyotokea juzi Mkoani Mwanza kisiwa cha Ukala.
Kwa mujibu Waziri Mwalimu usambazaji wa picha hizo zinaongeza majonzi kwa ndugu na waathirika wa tukio la ajali ya Mv-Nyerere badala yake amewataka watanzania kutumia nafasi hiyo kuwaombea.
Ummy Mwalimu ameeleza hayo kupitia ukurasa wa Twitter.
"Ndugu zangu Watanzania, ninawaomba sana TUACHE KUSAMBAZA NA KUPOSTI PICHA ZA MAREHEMU WA AJALI YA MV NYERERE.
"Tuheshimu Utu na Ubinadamu wao. Lakini pia watu wapo kwenye majonzi makubwa ya kupoteza wapendwa wao, hivi kuna faida gani kwa baadhi yetu sisi kuposti picha hizi za marehemu?.
"Tafadhali tuwapunguzie maumivu familia, ndugu, jamaa na marafiki wa marehemu kwa kuto-posti picha hizi. Muhimu tuendelee kuwaombea familia za marehemu Mwenyezi Mungu awape subra na ustahamilivu ktk kipindi hiki kigumu. Aidha tuwaombee rehema wenzetu waliotangulia mbele ya haki. #MbeleYaoNyumaYetu "
aliimalizia Waziri Mwalimu.
No comments:
Post a Comment