Irene Uwoya Awaonya Wanaopiga Picha za Nusu Uchi
Msanii wa filamu nchini Irene Uwoya na mke halali wa mwanamuziki Dogo Janja amefunguka na kuwataka ma-star wenzake kuacha kutumia 'skendo' za kupiga picha nusu utupu kwa madai vitendo hivyo vinamchukiza hadi Mungu na si TCRA pekee.
Uwoya ametoa kauli hiyo alipokuwa anazungumza kna eNewz ya EATV, na kusema wanaofanya na vitendo hivyo wanajidhalilisha wao wenyewe bila ya kujijua.
"Mimi nadhani kuna kitu watu hawajui au hawakitambui, kuwa kuna tofauti ya kutaka kuwa 'star' na kufanya kitu ambacho unakipenda ambacho kitakupelekea kuwa 'star' moja kwa moja", amesema Uwoya.
Pamoja na hayo, Uwoya ameendelea kwa kusema "mimi nawashauri watanzania kama kuna mtu anataka kuwa muigizaji basi afuate misingi iliyowekwa nasio kupiga picha za nusu utupu kwa kuwa haitoweza kumfanya mtu kuwa star na badala yake inakushusha. Wanaopiga picha za nusu utupu wanajidhalilisha kiukweli maana hata Mungu hapendi".
Kauli hiyo ya Irene Uwoya imekuja baada ya kupita takribani siku 36 tokea alipopigwa onyo na Kamati ya Maudhui ya Mamlaka ya Mawasiliano (TCRA), kuhusiana na kuchapisha picha za nusu utupu kwenye mitandao ya kijamii na kusisitiziwa kuwa endapo atarudia kufanya hivyo adhabu kali za kisheria zitachukuliwa dhidi yake.
No comments:
Post a Comment