Diamond, Rich Mavoko Wakutana Uso kwa Uso BASATA
Msanii wa Bongo Fleva, Rich Mavoko na lebo ya WCB wamekutana tena Baraza la Sanaa Taifa (BASATA).
Team ya WCB ilikuwa ikiongozwa na Diamond Platnumz pamoja na Sallam SK.
Pande hizo mbili ziliitwa na BASATA kwa lengo la majadiliano mara ya baada ya upande wa Rich Mavoko kulalamikia kile walichodai ni mkataba wa unyonyaji kutokea WCB.
Hata hivyo hadi pande zote mbili zinaondoka eneo la BASATA hazijaweka wazi ni kipi hasa kinaeendelea, hivyo wenye kauli ya kueleza yalipofikia mazungumzo hayo ni Baraza hilo lenyewe.
Mavoko alijiunga na WCB mwaka 2016 akisaini chini ya lebo hiyo na kuanza kufanya kazi akiwa chini ya lebo hiyo ambayo boss wake ni Diamond Platinumz.
Baada ya kujiunga na lebo hiyo Mavoko alianza malalamiko mapema mwaka huu kuwa anataka kujitoa katika lebo hiyo ya WCB wasafi kwa madai kwamba ananyonywa kimaslahi.
Mbali na kunyonywa kimaslahi lakini pia ilidaiwa kuwa kuna vitu ndani ya makataba huo msanii huyo hakutimiziwa na boss wake kama mkataba ulikuwa unaelekeza.
Malalamiko ya Mavoko yalionekana kuwagusa wengi na ikachangia Mavoko kukaa kimya kwa muda ingawa siku za hivi karibuni aliachia ngama yake mpya inayokwenda kwa jina la Ndegele.
Katika moja ya mahojiano aliyofanya meneja wa Diamond Salam Sk katika moja ya Redio hapa nchini alipoulizwa kuhusiana na madai haya ya mavoko alisema “Mavoko bado ni msanii wa WCB na hayo malalamiko anayotoa sisi hatujui yanahusiana na nini kwani huduma zote wanazopatiwa wasanii wa WCB anazipata”
Meneja huyo aliongeza “Kabla ya mavokonkusaini mkataba alipewa akakae nao aupitie hadi ajirizishe na Mavoko alifanya hivyo na kukaa nao ndani ya wiki mbili ndio akaurizia mwisho wa siku akaja kusaini sasa anacholalamika ni nini? sisi hatujui kwani makataba huo una kurasa 10 kwahiyo hatujui ni kitu gani anataka haswa”
Baada ya Mavoko kupeleka malalamiko hayo Basata,Basata nao waliamua kuwaita Maboss wa WCB walipofika wakaongea nao na ndio wakakubaliana wakutane siku ya leo August 23 katika ofisi hizo hapa Jijini Dar Es Salaam.
Irene Uwoya Awaonya Wanaopiga Picha za Nusu Uchi
Irene Uwoya Awaonya Wanaopiga Picha za Nusu Uchi
Msanii wa filamu nchini Irene Uwoya na mke halali wa mwanamuziki Dogo Janja amefunguka na kuwataka ma-star wenzake kuacha kutumia 'skendo' za kupiga picha nusu utupu kwa madai vitendo hivyo vinamchukiza hadi Mungu na si TCRA pekee.
Uwoya ametoa kauli hiyo alipokuwa anazungumza kna eNewz ya EATV, na kusema wanaofanya na vitendo hivyo wanajidhalilisha wao wenyewe bila ya kujijua.
"Mimi nadhani kuna kitu watu hawajui au hawakitambui, kuwa kuna tofauti ya kutaka kuwa 'star' na kufanya kitu ambacho unakipenda ambacho kitakupelekea kuwa 'star' moja kwa moja", amesema Uwoya.
Pamoja na hayo, Uwoya ameendelea kwa kusema "mimi nawashauri watanzania kama kuna mtu anataka kuwa muigizaji basi afuate misingi iliyowekwa nasio kupiga picha za nusu utupu kwa kuwa haitoweza kumfanya mtu kuwa star na badala yake inakushusha. Wanaopiga picha za nusu utupu wanajidhalilisha kiukweli maana hata Mungu hapendi".
Kauli hiyo ya Irene Uwoya imekuja baada ya kupita takribani siku 36 tokea alipopigwa onyo na Kamati ya Maudhui ya Mamlaka ya Mawasiliano (TCRA), kuhusiana na kuchapisha picha za nusu utupu kwenye mitandao ya kijamii na kusisitiziwa kuwa endapo atarudia kufanya hivyo adhabu kali za kisheria zitachukuliwa dhidi yake.
Mwanamke Atiwa Mbaroni Kwa Kumuua Mwanae na Mwingi kwa Kumuwekea Mwiko Sehemu za Siri
Wanawake
wawili wanashikiliwa na polisi mkoani Morogoro kwa tuhuma mbalimbali
akiwamo mmoja aliyemuua mtoto wake wa kiume wa miaka 11 kwa kumpiga
fimbo kichwani.
Katika
tukio jingine mwanamke mwingine anashikiliwa na polisi akituhumiwa
kumsokomeza mwiko sehemu za siri mtoto wa dada yake mwenye umri wa miaka
sita.
TCU: Kesho Ndo Mwisho wa Kutuma Maombi ya Kujiunga Chuo Kikuu Shahada ya Kwanza
Tume
ya vyuo Vikuu Tanzania (TCU) imesema kuwa kesho Agosti 15, 2018 ndiyo
mwisho wa kutuma maombi ya kujiunga na masomo ya shahada ya kwanza
katika vyuo vikuu na taasisi za elimu ya juu nchini.
Dirisha hilo la kuwasilisha maombi lilifunguliwa Julai 20, 2018 kwa awamu ya kwanza.
Akizungumza
leo Agosti 14, 2018 Katibu Mtendaji wa TCU Profesa Charles Kihampa
amesema kuwa baada ya kufungwa rasmi kwa dirisha la udahili vyuo
vitaanza kuchakata majina ya waombaji kulingana na vigezo vya udahili
vilivyowekwa kwa kila programu ya masomo.
Udahili
wa kujiunga na vyuo vikuu unahusu makundi makubwa matatu ambayo ni
waombaji wa kidato cha sita, wenye sifa linganifu kama vile shahada na
waombaji wenye vyeti toka nje ya nchi vyenye sifa linganifu.
"Baada ya kuchakata majina, dirisha la waombaji litaidhinishwa, " amesema Kihampa na kuongeza:
"TCU
jukumu lao ni kuhakiki kama waombaji waliochaguliwa na vyuo wana sifa
stahiki na wanakidhi vigezo vya kujiunga na programu husika za
masomo,"amesema Profesa Kihampa.
Amefafanua
kuwa waombaji wote wa udahili wanapaswa kutuma maombi yao moja kwa moja
kwenye vyuo wanavyopenda na kuchagua programu za masomo.
Amesema
Tume imetoa mwongozo wa programu zilizoidhinishwa kudahili pamoja na
vigezo vya udahili vinavyotakiwa kwa kila programu za masomo.
"Waombaji
wote wa vyuo vikuu na taasisi ya elimu ya juu wanakumbushwa na
kuhimizwa kuzingatia kalenda ya udahili iliyoidhinishwa na Tume,"amesema
Kihampa na kuongeza:
"Ili kuepusha usumbufu usio wa lazima, waombaji wote wanahimizwa kutumia muda uliobaki kukamilisha maombi yao.”
Wolper: Siwezi kudanga na siku nikikamata mmoja ni mimba tu
Msanii
wa Filamu Bongo, Jackline Wolper amesema kitu ambacho hawezi kufanya ni
kudanga. Wolper amefunguka hayo wakati akimjibu shabiki yake katika
mtandao wa Instagram kufuatia mrembo huyo kuposti picha ya Rais wa Kenya
na kuandika; My second home.
Sasa shabiki huyo alitupia comment yake kwenye post hiyo ambayo ilisomeka; "Siku Wakenya Watakukata ki******m ndo utajua ni second home au ni neighbor country we endeleaa tu kudangaaaa kwa waikikuyu"
Naye Jackline Wolper akajibu; "Siwezi
kudanga na siku nikikamata mmoja ni mimba tu usijali, halafu kasome
ujue maana ya kudanga.. na me kudanga siwezi, wanadanga watoto, am
sorry".
Jackiline
Wolper amekuwa nafari za mara kwa mara nchini Kenya kutokana na
biashara zake hasa ile ya ushonaji kupitia duka lake la House of
Stylish.
Kauli ya Rais Magufuli Yamuumiza Kichwa Makonda
Mkuu
wa Mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda ameitisha kikao na wakurugenzi
wa manispaa zote za mkoa kwalengo la kupitia takwimu za mapato na
matumizi ya mkoa huo ili kujiridhisha kwanini wameshuka kimapato na
kuzidiwa na jiji la Dodoma ambalo limepandishwa hadhi hivi karibuni.
Makonda
ametoa kauli hiyo leo Agosti 3, 2018 katika hafla ya kuwakaribisha
wakuu wa wilaya wapya na kuwaaga waliohamishwa vituo vya kazi, ambapo
amemtaka katibu tawala wa mkoa kuipanga upya Idara ya Ardhi kwani ni
maeneo yenye uongo mwingi na imekuwa na viongozi ambao wanachukuwa
nyaraka za wananchi na kisha kuwapelekea matajiri na kuwanyima haki
wanyonge.
“Haiingii
akilini Mkoa wa Dar es Salaam kushuka kimapato pamoja na kuzidiwa
ukusanyaji kodi wakati ni mkoa wa kiuchumi, kuna nyumba na viwanja vya
serikali ambavyo vimechukuliwa na watu binafsi, mikataba ya unyonyaji
ambayo imesainiwa na inaiminya serikali”, amesema
Makonda
ameongeza kuwa viongozi wengi wa Dar es Salaam wanatoa taarifa nyingi
za uongozi juu ya utendaji na utekekezaji wa miradi na mfumo wa biashara
pia uangaliwe ili kuiwezesha kuwepo kwa mfumo rahisi ambao unarahisisha
huduma za kitengo cha biashara kwani kumekuwa na urasimu uliopitiliza.
“Katika
suala la ulinzi na usalama, wanaendelea na kuweka Camera katika maeneo
mbalimbali ya jiji na baada ya hapo tutaruhusu ufanyaji wa biashara kwa
masaa24”, ameongeza Makonda.
Agosti
1, 2018 wakati akizungumza na wakuu wa mikoa baada ya kuwaapisha
viongozi mbalimbali aliowateua, Rais Magufuli alisema kati ya majiji
yote, Dodoma inaongoza kwa makusanyo ya mapato ya Shilingi bilioni 24.2
ikiwa ni asilimia 123 ya makisio yao ya Shilingi bilioni 19.
Amesema
Jiji la Dar es Salaam ambalo ni kongwe kuliko yote lilikusanya pesa
kidogo tofauti na ukubwa wake ambapo lilikusanya kiasi cha Sh15.3
bilioni, Arusha (Sh10.3 bilioni), Mwanza (Sh9.3bilioni), Tanga
(Sh9.1bilioni) na Mbeya (Sh4.2bilioni).
Lulu Diva Adai Anamiliki Gari La Thamani Kuliko Wasanii Wote Tanzania
Lulu Diva Adai Anamiliki Gari La Thamani Kuliko Wasanii Wote Tanzania
Aliyewahi kuwa video vixen na sasa ni msanii wa muziki wa bongo fleva, Lulu Diva anae hit na ngoma yake ya 'Ona' amefunguka kuwa yeye ni msanii pekee anaemiliki gari ya thamani Tanzania nzima.
Akipiga
story Ayo tv, Lulu Diva, amefunguka na kusema kuwa hana mpango wa
kubadilisha gari kwa sababu gari lake ni zuri na lina thamani kuliko
magari ya wasanii wote Tanzania.
“Hapana
sina mpango wa kubadilisha gari lakini nitabadiisha rangi kwa sababu
sijaona gari ambayo ninaweza nikabadilisha tofauti na Jeep naipenda
sana, halafu pia katika wasanii wote mimi peke yangu ndio nina gari
nzuri halafu la thamani nyie wenyewe mkiangalia mnaona na sio kitu
ambacho naongea ili kujisifia ila am proud of myself” alisema Lulu Diva
huku akiongeza kwa kusema kuwa gari hilo hajanunuliwa na mwanaume bali
kanunua mwenyewe kutokana na juhudizake binafsi za kimziki, biashara na
ukulima wa kahawa.
Mfanyabiashara Davis Mosha akamatwa na Askari wa Uhamiaji
Mfanyabiashara Davis Mosha akamatwa na Askari wa Uhamiaji
Mfanyabiashara Davis Mosha
alikamatwa Agosti Mosi, 2018 kwa madai ya kuwazuia askari wa Idara ya
Uhamiaji kutekeleza majukumu yao na bado anaendelea kushikiliwa kwa
hatua zaidi.
Msemaji
Mkuu wa Idara ya Uhamiaji, Ali Mtanda amesema Mosha aliwashambulia
askari hao na kumnyang’anya mmoja wao simu ya mkononi baada ya kufika
katika jengo la Delina lililopo Sinza Mori.
“Askari walifika kwenye majengo hayo na kujitambulisha kwa mlinzi na moja kwa moja walionyeshwa ofisi za meneja.
"Wakati
wakifanya mazungumzo ya kikazi na meneja huyo, ghafla akatokea Mosha na
kuanza kuwafokea, kisha kuwashambulia na kumnyang’anya askari mmoja
simu yake.” –Mtanda
Amesema
alichofanya Mosha ni kinyume cha sheria ya uhamiaji namba 54 kifungu
cha 45 kipengele 1 F, kinachozungumzia kumzuia ofisa wa uhamiaji kufanya
kazi yake ya ukaguzi.
Mtanda amesema bado wanamshikilia Mosha kwa uchunguzi zaidi na kama kuna hatua nyingine zitafuata watatoa taarifa.
Mtanda amesema bado wanamshikilia Mosha kwa uchunguzi zaidi na kama kuna hatua nyingine zitafuata watatoa taarifa.
Bill Nass amshauri Steve Nyerere kufungua kampuni ya kusimamia misiba
Bill Nass amshauri Steve Nyerere kufungua kampuni ya kusimamia misiba
Msanii
wa Bongo Flava, Bill Nass amemshauri muigizaji Steve Nyerere kufungua
kampuni ya kusimamia misiba kwa sababu ni kazi anayoiweza zaidi.
Bill
Nass akipiga stori na Wasafi TV amesema kuliko Steve Nyerere kutumia
fedha zake kuandaa event za comedy ni bora akafanya hivyo na anaweza
kupata fedha nyingi zaidi.
"Kuliko
kuwekeza fedha zake sijui kuandaa comedy kubwa anaweza akafungua
kampuni za kushughulika na misiba na akatengeneza fedha," amesema Bill
Nass.
"Anaweza
akatumia mtaji huo huo mdongo akanunua gari za kubebea maiti, akawa na
vitu ambavyo vina-deal na hiyo fild kwa sababu anaiweza sana,"
ameongeza.
Bill Nass kwa sasa anatamba na wimbo wake mpya unaokwenda kwa jina la Labda.
Ajali Yaua Watu Wanne Dodoma huku Watatu Wakiwa ni wa Familia Moja
Ajali Yaua Watu Wanne Dodoma huku Watatu Wakiwa ni wa Familia Moja
Watu wanne wamefariki dunia watatu wakiwa ni wa familia katika ajali iliyohusisha gari na pikipiki.
Akizunguma
na wanahabari jana Agosti 2, Kamanda wa Polisi mkoani Dodoma Gilles
Muroto, alisema ajali hiyo imetokea usiku wa kuamkia jana wilayani Bahi,
Dodoma kwenye barabara kuu ya Singida-Dodoma.
Waliofariki
ni watoto Yusra Salum (5), Karialino Hamis (2), Hussein Hamisi (miezi
miwili) na Mfaume Hamis (30) ambaye alikuwa dereva wa bodaboda.
Kamanda
Muroto amesema mwendesha pikipiki huyo alikuwa amewapakia watoto watatu
na mama yao na aliingia barabarani ghafla na pikipiki hiyo iligongwa na
basi la kampuni ya Satco.
Muroto ameeleza kuwa basi hilo lilikuwa likitokea Mwanza kuelekea jijini Dar es salaam.
“Kwenye
hiyo pikipiki walikuwa wamepanda jumla ya watu watano, watoto watatu na
mama yao dereva amefariki dunia papo hapo na watoto watatu mama huyo na
mama mwenyewe naye ni majeruhi hospitali,”alisema.
Bodi ya Mikopo Yasema Wanafunzi 17,000 Kati ya Wote Waliotuma Maombi Hawajakidhi Vigezo vya Kupatiwa Mikopo
Bodi ya Mikopo Yasema Wanafunzi 17,000 Kati ya Wote Waliotuma Maombi Hawajakidhi Vigezo vya Kupatiwa Mikopo
Imeelezwa
kuwa zaidi ya wanafunzi 17,303 hawajakidhi vigezo vya kupatiwa mikopo
ya elimu ya juu na Bodi ya Mikopo nchini kutokana na kutokamilisha
viambata muhimu vinavyohitajika hali iliyopelekea kuongezwa siku
nyingine 15.
Afisa
Mawasiliano mwandamizi kutoka Bodi ya Mikopo, Veneranda Malima amesema
kuwa mpaka kufikia Julai 31, 2018 ambapo ndiyo ilikuwa tarehe ya mwisho
kwa wanafunzi kutuma maombi kwa ajili ya kupatiwa mkopo, wanafunzi
88,502 walituma maombi na 78,290 pekee ndio waliokidhi vigezo mpaka
sasa.
Kufuatia
takwimu hizo zaidi ya wanafunzi 17,303 hawajakamilisha vitu muhimu vya
kuambatanisha katika fomu za kuomba mikopo ikiwemo vyeti vya kuzaliwa na
vitambulisho vya wadhamini hivyo kupelekea bodi kuongeza muda wa siku
kumi na tano.
“Kwasasa
hatupokei maombi mapya, lakini muda tulioongeza ni kwa wale waombaji
ambao hawakukamilisha viambatanisho muhimu kutokana na wengi kutokuweka
vyeti vya kuzaliwa na vitambulisho vya wadhamini”, amesema Malima.
Mei
10, 2018 Bodi ya mikopo ilianza rasmi kupokea maombi kutoka kwa
wanafunzi waliochaguliwa kujiunga na elimu ya juu na tarehe 31 Julai,
2018 Bodi ilifunga zoezi la udahili wa mikopo kwa wanafunzi wa elimu ya
juu nchini.
Kiasi
cha shilingi Bilioni 427.5 kimetengwa kwa ajili ya mikopo ya wanafunzi
wa elimu ya juu kwa mwaka 2018/2019 ambazo ni kwa wanafunzi wenye
mikopo hivi sasa , na waombaji wapya ambao wana sifa za kujiunga na kozi
za shahada katika vyuo vikuu nchini.