Bodi ya Mikopo Yasema Wanafunzi 17,000 Kati ya Wote Waliotuma Maombi Hawajakidhi Vigezo vya Kupatiwa Mikopo
Imeelezwa
kuwa zaidi ya wanafunzi 17,303 hawajakidhi vigezo vya kupatiwa mikopo
ya elimu ya juu na Bodi ya Mikopo nchini kutokana na kutokamilisha
viambata muhimu vinavyohitajika hali iliyopelekea kuongezwa siku
nyingine 15.
Afisa
Mawasiliano mwandamizi kutoka Bodi ya Mikopo, Veneranda Malima amesema
kuwa mpaka kufikia Julai 31, 2018 ambapo ndiyo ilikuwa tarehe ya mwisho
kwa wanafunzi kutuma maombi kwa ajili ya kupatiwa mkopo, wanafunzi
88,502 walituma maombi na 78,290 pekee ndio waliokidhi vigezo mpaka
sasa.
Kufuatia
takwimu hizo zaidi ya wanafunzi 17,303 hawajakamilisha vitu muhimu vya
kuambatanisha katika fomu za kuomba mikopo ikiwemo vyeti vya kuzaliwa na
vitambulisho vya wadhamini hivyo kupelekea bodi kuongeza muda wa siku
kumi na tano.
“Kwasasa
hatupokei maombi mapya, lakini muda tulioongeza ni kwa wale waombaji
ambao hawakukamilisha viambatanisho muhimu kutokana na wengi kutokuweka
vyeti vya kuzaliwa na vitambulisho vya wadhamini”, amesema Malima.
Mei
10, 2018 Bodi ya mikopo ilianza rasmi kupokea maombi kutoka kwa
wanafunzi waliochaguliwa kujiunga na elimu ya juu na tarehe 31 Julai,
2018 Bodi ilifunga zoezi la udahili wa mikopo kwa wanafunzi wa elimu ya
juu nchini.
Kiasi
cha shilingi Bilioni 427.5 kimetengwa kwa ajili ya mikopo ya wanafunzi
wa elimu ya juu kwa mwaka 2018/2019 ambazo ni kwa wanafunzi wenye
mikopo hivi sasa , na waombaji wapya ambao wana sifa za kujiunga na kozi
za shahada katika vyuo vikuu nchini.
No comments:
Post a Comment