Mkuu
wa Mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda ameitisha kikao na wakurugenzi
wa manispaa zote za mkoa kwalengo la kupitia takwimu za mapato na
matumizi ya mkoa huo ili kujiridhisha kwanini wameshuka kimapato na
kuzidiwa na jiji la Dodoma ambalo limepandishwa hadhi hivi karibuni.
Makonda
ametoa kauli hiyo leo Agosti 3, 2018 katika hafla ya kuwakaribisha
wakuu wa wilaya wapya na kuwaaga waliohamishwa vituo vya kazi, ambapo
amemtaka katibu tawala wa mkoa kuipanga upya Idara ya Ardhi kwani ni
maeneo yenye uongo mwingi na imekuwa na viongozi ambao wanachukuwa
nyaraka za wananchi na kisha kuwapelekea matajiri na kuwanyima haki
wanyonge.
“Haiingii
akilini Mkoa wa Dar es Salaam kushuka kimapato pamoja na kuzidiwa
ukusanyaji kodi wakati ni mkoa wa kiuchumi, kuna nyumba na viwanja vya
serikali ambavyo vimechukuliwa na watu binafsi, mikataba ya unyonyaji
ambayo imesainiwa na inaiminya serikali”, amesema
Makonda
ameongeza kuwa viongozi wengi wa Dar es Salaam wanatoa taarifa nyingi
za uongozi juu ya utendaji na utekekezaji wa miradi na mfumo wa biashara
pia uangaliwe ili kuiwezesha kuwepo kwa mfumo rahisi ambao unarahisisha
huduma za kitengo cha biashara kwani kumekuwa na urasimu uliopitiliza.
“Katika
suala la ulinzi na usalama, wanaendelea na kuweka Camera katika maeneo
mbalimbali ya jiji na baada ya hapo tutaruhusu ufanyaji wa biashara kwa
masaa24”, ameongeza Makonda.
Agosti
1, 2018 wakati akizungumza na wakuu wa mikoa baada ya kuwaapisha
viongozi mbalimbali aliowateua, Rais Magufuli alisema kati ya majiji
yote, Dodoma inaongoza kwa makusanyo ya mapato ya Shilingi bilioni 24.2
ikiwa ni asilimia 123 ya makisio yao ya Shilingi bilioni 19.
Amesema
Jiji la Dar es Salaam ambalo ni kongwe kuliko yote lilikusanya pesa
kidogo tofauti na ukubwa wake ambapo lilikusanya kiasi cha Sh15.3
bilioni, Arusha (Sh10.3 bilioni), Mwanza (Sh9.3bilioni), Tanga
(Sh9.1bilioni) na Mbeya (Sh4.2bilioni).
No comments:
Post a Comment