Albert Msando Ajiuzulu......Ni Baada ya Video Yake Chafu Kuvuja Mtandaoni

Aliyekuwa mshauri wa Chama cha ACT Wazalendo, Albert Msando amejiuzulu nafasi yake hiyo kufuatia video chafu zilizomuhushisha kuvuja kwenye mitandao ya kijamii hivyo ameamua kujiuzulu ili kuwajibika na kuomba radhi kwa wananchi kwa kitendo hicho
Kiongozi wa Chama Cha ACT Wazalendo Zitto Kabwe, amethibitisha kupokea barua hiyo na kukubaliana na kiongozi huyo kwa kitendo chake hicho cha kuwajibika kisiasa huku akieleza kuwa, Bw. Msando amekuwa na mchango mkubwa katika Chama chao.
"Nimepokea barua ya Wakili Albert G. Msando kuomba kujiuzulu nafasi yake ya Ushauri wa Chama chetu cha ACT Wazalendo. Ndugu Msando anawajibika Kwani anapaswa, nanukuu kutoka katika barua yake, "kuishi Kama mfano Kwa jamii inayonizunguka".
"Ndugu Albert Msando amekuwa kiongozi mwenye mchango mkubwa katika chama katika nafasi mbalimbali alizoshika ndani ya chama. Chama kinamshukuru kwa moyo wake wa uzalendo na mchango alioutoa katika Chama. Ni matumaini yetu ataendelea kushirikiana nasi katika ujenzi wa chama kwa kadri atakavyoweza na atakapohitajika kama mwanachama"- alisema Zitto Kabwe.
Zitto Kabwe pia ametumia nafasi hiyo kuwaomba wananchi wamsaidie katika jambo hilo analopitia saizi
"Nikiwa Kiongozi wa Chama nimekubali kuwajibika kwake na kumtakia kheri katika kujisahihisha kwake. Ndugu Msando Alberto ameomba msamaha Kwa jamii kwa uwazi na ni wajibu wetu kumsaidia kupita katika mitihani iliyomkumba" alimaliza Zitto Kabwe.
Rais Magufuli Atapokea Taarifa ya Kamati Maalum ya kuchunguza mchanga Saa Tatu Asubuhi Hii

Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais, inawataarifu wananchi wote kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli leo tarehe 24 Mei, 2017 atapokea Taarifa ya Kamati Maalum aliyoiunda kuchunguza mchanga ulio katika makontena ya mchanga wa madini (Makinikia) yaliyopo katika maeneo mbalimbali hapa nchini Tanzania.
Tukio la kupokea taarifa hiyo litahudhuriwa na viongozi mbalimbali na kurushwa moja kwa moja kupitia vituo vya habari vya redio, televisheni na tovuti rasmi ya Ikulu ambayo ni www.ikulu.go.tz
Wananchi mnakaribishwa kutazama na kusikiliza matangazo hayo yatakayorushwa hewani kuanzia saa 3.30 Asubuhi kutoka Ikulu Jijini Dar es Salaam.
Waziri Mkuu atembelea kiwanda cha kuunganisha matrekta wilayani Kibaha na Kuagiza Wakulima Wakopeshwe Ili Waweze Kununua Matrekta

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amezitaka benki mbalimbali nchini ikiwemo Benki ya Maendeleo ya Kilimo kutoa mikopo kwa vikundi vya kilimo ili viweze kupata fedha za kununulia matrekta.
Amesema Serikali imedhamiria kuimarisha Sekta ya kilimo ili kwenda sambamba na adhma yake ya kuwa nchi ya uchumi wa viwanda.
Waziri Mkuu ameyasema hayo jana Jumanne, Mei 23, 2017 wakati alipotembelea kiwanda cha kuunganisha Matrekta URSUS-TAMCO, Kibaha mkoani Pwani.
Alisema kiwanda hicho kinalenga kuboresha sekta ya kilimo nchini na kuongeza uzalishaji wa malighafi za viwandani kwa kuwa wakulima watakuwa na zana za kisasa.
Aidha, amevitaka vyuo vya kilimo nchini kununua matrekta hayo kwa lengo la kufundishia wanafunzi wake ili wanapohotimu wawe na uwezo wa kutumia zana hizo vizuri na kwenda kuwasaidia wakulima katika maeneo yao.
Pia Waziri Mkuu alitoa wito kwa Halmashauri nchini kuendelea kupanga matumizi bora ya ardhi kwa kutenga maeneo ya kilimo, uwekezaji, makazi, biashara na huduma za jamii, hivyo kuepuka migogoro ya ardhi kwa siku zijazo.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Maendeleo la Taifa (NDC) Bw. Mlingi Mkucha alisema wataunganisha matrekta 2,400, harrow 2,400 na majembe 2,400 katika mradi huo wa kiwanda cha kuunganisha matrekta URSUS-TAMCO ikiwa ni mkataba wa awali.
Alisema kiwanda hicho kina wafanyakazi 27 kwa hatua za mwanzo. Aidha, idadi hiyo itaongezeka kutokana na mahitaji ambapo baadhi ya wafanyakazi watapewa mafunzo nchini Poland na watakaporudi watakuwa wakufunzi wa watakaoajiriwa.
Mkurugenzi huyo aliongeza kuwa kiwanda hicho kimeazima wafanyakazi wengine wakiwemo watano kutoka Wizara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi, 10 kutoka vyuo mbalimbali vya ufundi nchini, wawili kutoka CAMARTEC ambao wanashirikiana na wataalamu 10 kutoka URSUS kuunganisha matrekta.
Bw. Mkucha alisema wafanyakazi 10 kutoka Tanzania wanatarajiwa kwenda nchini Poland kufanya mafunzo mahsusi na watakaporejea watakuwa wakufunzi kwa watumishi wengine watakaoajiriwa katika kiwanda hicho.
Alisema mbali na ujenzi wa kiwanda hicho cha kuunganishia matrekta ya URSUS, mradi unahusisha uanzishwaji wa vituo vinane kwa ajili ya kutoa huduma kwa wateja na kuuzia matrekta, zana na vifaa vingine.
Naye Mkuu wa Mkoa wa Pwani Mhandisi Everest Ndikilo alisema miongoni mwa changamoto zinazoikabili sekta ya viwanda mkoani humo ni pamoja na kukatika kwa umeme, hivyo ameliomba Shirika la Umeme Tanzania (TANECO) kuongeza vituo vya kupozea umeme.
Awali Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Mheshimiwa Charles Mwijage alisema kwa sasa nchini kuna viwanda vikubwa 393 kati yake 84 viko mkoani Pwani, ambapo amewaomba viongozi wa mkoa huo kutenga maeneo kwa ajili ya wanawake na vijana kuanzisha viwanda vidogo.
Mara baada ya kutembea kiwanda cha kuunganisha matrekta URSUS-TAMCO Waziri Mkuu alitembelea eneo la uwekezaji la Kamal (Kamal Indusrial Estate) lililoko katika Kata ya Kerege wilayani Bagamoyo.

Rais Magufuli Afanya Uteuzi wa Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI- Elimu)

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli leo tarehe 24 Mei, 2017 amemteua Bw. Tixon Tuliangine Nzunda kuwa Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) - anayeshughulikia Elimu.
Kabla ya uteuzi huo Bw. Tixon Tuliangine Nzunda alikuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Rukwa.
Bw. Tixon Tuliangine Nzunda anachukuwa nafasi ya aliyekuwa Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) - akishughulikia Elimu Bw. Bernard Makali ambaye ameteuliwa kuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Rukwa.
Uteuzi huu unaanza mara moja.
Gerson Msigwa
Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU
Dar es Salaam
24 Mei, 2017
LIVE: Rais Magufuli Anapokea Ripoti ya Madini Katika Makontena ya Mchanga

Breaking News Rais Magufuli amtaka Waziri Prof. Muhongo ajiuzulu

Rais John Magufuli amemtaka Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo kuachia madaraka kwa kushindwa kusimamia suala la mchanga wa dhahabu unaosafirishwa kwenye makontena.
Amemtaka waziri huyo kujitathimini na bila kuchukua muda mrefu aachie madaraka kutokana na suala hilo.
Rais Magufuli amesema hayo baada ya kamati iliyokuwa ikichunguza suala la mchanga kwenye makontena kukabidhi ripoti yao.
Kamati hiyo ya wataalamu wa jiolojia na uchambuzi wa kisayansi iliyoundwa Machi 29 mwaka huu, ilichunguza aina ya madini yaliyopo, kiasi na viwango vya ubora.
Akikabidhi ripoti hiyo, Profesa Mruma amesema uchunguzi huo umebaini uwepo wa madini ya kiasi cha kati ya Sh829.4 bilioni mpaka 1.439 Trillion kwa makontena yote 277.
"Licha ya uchunguzi uliofanywa kupitia makontena haya, tumegundua uwepo wa aina nyingi zaidi za madini ambayo hayakuwa yakijulikana na haya yamekutwa na thamani ya kati Sh129.5 bilioni mpaka261 bilioni," amesema Profesa Mruma.