TANZIA: Dogo Mfaume Hatunaye Tena
Msanii wa muziki wa bongo fleva, Dogo Mfaume ambaye aliwahi kutamba na nyimbo kama 'Kazi Yangu Ya Dukani' amefariki dunia jana katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili alipokuwa akiendelea kupatiwa matibabu.
Dogo Mfaume alitumbukia kwenye janga la madawa ya kulevya na baadaye kuanza kupata matibabu ya kuondokana na matumizi ya madawa hayo kupitia kituo cha "Back to Life Sober House" kinachoendeshwa na Pilli Missana kilichopo Kigamboni Dar es Salaam.
Mungu amlaze mahali pema peponi Dogo Mfaume.
Jikumbushe na moja ya kazi yake hapo chini
No comments:
Post a Comment