Matokeo ya uchaguzi wa wabunge wa CHADEMA Bunge la Afrika Mashariki
Bunge la Tanzani jana limepiga kura na kuwachagua wabunge wawili wa CHADEMA watakaoungana na wenzao 7 kutoka CUF na CCM kwa ajili ya kuiwakilisha Tanzania katika Bunge la Afrika Mashariki (EALA).
Uchaguzi huo wa wabunge wa CHADEMA ulirudiwa jana baada ya wagombea wa kwanza kukataliwa bungeni kwa kupigiwa kura ya hapana kwa kile kilichoelezwa kuwa hawakuwa wamekidhi vigezo.
Katika uchaguzi wa jana, wabunge wawili waliochaguliwa ni Josephine Sebastian Lemoyan na Pamela Pamela Maasay.
Katika kinyang’anyiro hicho wagombea wengine walikuwa nia Ezekiel Wenje, Lawrence Masha, Salum Mwalimu na Prof. Safari.
==>Matokeo ni kama ifuatavyo;
1.Abdallah Safari- kura 35.
2-Wenje -kura 34
3-Lawrence Masha -kura 44
4-Salim Mwalimu -kura 54
5- Josephine Lemoyan -kura 219
6-Pamela Maasay kura -200.
2-Wenje -kura 34
3-Lawrence Masha -kura 44
4-Salim Mwalimu -kura 54
5- Josephine Lemoyan -kura 219
6-Pamela Maasay kura -200.
Kufuatia ushindi wa wagombea hao wawili, wabunge wa Bunge la Afrika Mashariki sasa wanafikia 9 ambapo 5 ni wanawake na 4 ni wanaume.
==>Wabunge tisa wa Tanzania katika Bunge las Afrika Mashariki ni;
- Fancy Nkuhi (CCM)
- Happiness Legiko (CCM)
- Maryam Ussi Yahya (CCM)
- Dkt Abdullah Makame (CCM)
- Dkt Ngwaru Maghembe (CCM)
- Alhaj Adam Kimbisa (CCM)
- Habib Mnyaa (CUF)
- Josephine Sebastian Lemoyan (CHADEMA)
- Pamela Pamela Maasay (CHADEMA).
No comments:
Post a Comment