Watu Wawili wanaodaiwa ni wapenzi wauawa kwa kuchomwa moto Arusha

Watu Wawili wanaodaiwa ni wapenzi wauawa kwa kuchomwa moto Arusha

Watu wawili wanaodhaniwa ni wapenzi,  wameuawa kwa kuchomwa moto baada ya kufungwa kamba wakiwa kitandani, katika  tukio lililotokea eneo la Whiterose lililoko kata ya Kiranyi wilayani Arumeru mkoani  Arusha.

Mamia ya watu wamejitokeza  kuzunguka nyumba lilipotokea tukio hilo baada ya kuona moshi ukitoka katika moja ya chumba na kuonekana miili ikiwa imeteketea kwa moto.
 
Kamanda wa polisi mkoa wa Arusha,Charles Mkumbo amesema tuki hilo limetoke jana, Jumanne saa 3.00 asubuhi

Amesema aliyekutwa amefariki ni  Maurine Urio (32)  pamoja na rafiki yake huyo ambaye hajaweza kutambulika kutokana na kuungua sana.

“Tumepata taarifa asubuhi hii kuwa kuna nyumba inaungua na polisi pamoja na zimamoto walifika eneo la tukio na kukuta watu hao wameshapoteza maisha wakiwa juu ya godoro ambako mwanaume alionekana kabla ya kuchomwa alifungwa kamba miguu na mikono ili kuzibitiwa,”amesema.

Mkumbo amesema miili ya marehemu imehifadhiwa katika chumba cha kuhifadhia maiti katika hospitali ya mkoa Mount Meru huku wahusika wa tukio hilo wakiwa wanatafutwa.

Akizungumzia tukio hilo mwenyekiti wa mtaa wa Ilkiurei iliyoko kata ya Kiranyi, Onesphory Chami amedai kuwa tukio hilo linahusishwa na wivu wa mapenzi.
Share:

No comments:

Post a Comment

Categories

Ordered List

  1. Lorem ipsum dolor sit amet, consectetuer adipiscing elit.
  2. Aliquam tincidunt mauris eu risus.
  3. Vestibulum auctor dapibus neque.

Sample Text

Lorem ipsum dolor sit amet, consectetur adipisicing elit, sed do eiusmod tempor incididunt ut labore et dolore magna aliqua. Ut enim ad minim veniam, quis nostrud exercitation test link ullamco laboris nisi ut aliquip ex ea commodo consequat.

Definition List

Definition list
Consectetur adipisicing elit, sed do eiusmod tempor incididunt ut labore et dolore magna aliqua.
Lorem ipsum dolor sit amet
Consectetur adipisicing elit, sed do eiusmod tempor incididunt ut labore et dolore magna aliqua.

Support

Need our help to upload or customize this blogger template? Contact me with details about the theme customization you need.

Pages