• This is default featured slide 1 title

    Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.This theme is Bloggerized by Lasantha Bandara - Premiumbloggertemplates.com.

  • This is default featured slide 2 title

    Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.This theme is Bloggerized by Lasantha Bandara - Premiumbloggertemplates.com.

  • This is default featured slide 3 title

    Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.This theme is Bloggerized by Lasantha Bandara - Premiumbloggertemplates.com.

  • This is default featured slide 4 title

    Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.This theme is Bloggerized by Lasantha Bandara - Premiumbloggertemplates.com.

  • This is default featured slide 5 title

    Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.This theme is Bloggerized by Lasantha Bandara - Premiumbloggertemplates.com.

Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Jumanne ya Octoba 17

Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Jumanne ya Octoba 17


Share:

Makamu wa Rais awaonya Trafiki wanaogeuza tochi kuwa mtaji

Makamu wa Rais awaonya Trafiki wanaogeuza tochi kuwa mtaji

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan amewaonya Polisi wa Kikosi cha Usalama Barabarani kuacha kugeuza vifaa vya kupimia mwendo wa magari maarufu kama tochi, kuwa chanzo cha wao kujipatia rushwa.

Mama Samia Suluhu ameyaeleza hayo jana wakati akifungua maadhimisho ya wiki ya nenda kwa usalama ambayo kitaifa yanafanyika mkoani Kilimanjaro.

Makamu wa Rais amewataka trafiki kujiepusha na vitendo vya rushwa na badala yake watilie mkazo katika ulinzi wa usalama na usimamizi wa sheria za barabarani.

Pia, amewataka kutowanyanyasa madereva ambao wanazingatia sheria za usalama barabarani.

Samia alieleza kuwa 76% ya ajali za barabarani huchangiwa na makosa ya kibinadamu ikiwamo madereva kuendesha magari huku wakitumia simu zao, uchovu unaosababisha madereva kusinzia, pamoja na kuendesha wakiwa walevi.

Aliendelea kwa kusema ubovu wa miundombinu ya barabara pamoja na ubovu wa magari nayo imechangia kutokea kwa ajali za barabarani kwa asilimia 16.

Vile vile alieleza kuwa kukosekana kwa umakini na uzembe wa madereva wa bodaboda kumepelekea kuongezeka kwa idadi ya ajali za barabarani ambako kungeweza kuepukika.

Samia amesema Taifa limeendelea kupoteza nguvu kazi, watu kupata ulemavu wa maisha na wengine kubaki wajane.

“Mwaka huu kuanzia Januari hadi Septemba kumekuwa na ajali za pikipiki 42,721 zilizoua watu 1,613 na kusababisha majeruhi 1,597,” amesema.

Amesema Mkoa wa Kilimanjaro umeripotiwa kuwa na ajali 84 za bodaboda zilizosababisha vifo 61 na majeruhi 21.

Samia ameeleza kusikitishwa kwa Tanzania kutajwa katika ripoti ya Shirika la Afya Duniani (WHO) kuwa ni nchi inayoongoza kwa ajali ikiwa na asilimia 33.

Ameliagiza Baraza la Taifa la Usalama Barabarani kushirikiana na Jeshi la Polisi Kikosi cha Usalama Barabarani na wadau kuzingatia na kuelekeza nguvu kwenye kudhibiti makosa makubwa matano hatarishi.

Makosa yaliyotajwa ni pamoja na mwendo kasi, ulevi, kutovaa kofia ngumu, kutovaa mikanda ya usalama katika gari na ukosefu wa vifaa vya usalama kuwalinda watoto wadogo wakiwa ndani ya gari.

Share:

Abiria wa Bodaboda na Mmliki Kuwajibishwa

Abiria wa Bodaboda na Mmliki Kuwajibishwa

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mwigulu Nchemba amewataka abiria nchini kuendelea kutii sheria za usalama barabarani vinginevyo itaundwa sheria ambayo itawawajibisha.

Waziri ameyasema hayo jana mjini Moshi Mkoani Kilimanjaro kwenye uzinduzi wa wiki ya Usalama Barabarani ambapo aligusia usafiri wa pikipiki maarufu kama Bodaboda.

“Sheria itabidi imtambue mmiliki kwenye kosa la dereva pikipiki kukosa kofia ngumu (Helmet) ili wote wawajibishwe na hapo ndio wamiliki watakuwa makini kuhakikisha vyombo vyao vina kofia ngumu mbili, ya dereva na abiria”, alisema Mwigulu.

Aidha waziri Mwigulu aliongeza kuwa kutokana na takwimu za ajali za Bodaboda kuna haja ya kutumia taratibu ama sheria ambayo itamuwajibisha abiria endapo hatavaa kofia ngumu hali ambayo itasaidia abiria kudai kofia kabla ya kupanda Pikipiki.

Usafiri wa Bodaboda umekuwa na msaada mkubwa maeneo ya mijini na vijijini lakini umekuwa ukitajwa kama chanzo kikubwa cha ajali za barabarani kutokana na madereva wake kutofuata sheria za barabarani.

Share:

Lulu Michael Kizimbani Kesho Kutwa Kesi ya Steven Kanumba

Lulu Michael Kizimbani Kesho Kutwa Kesi ya Steven Kanumba

Msanii maarufu wa kike wa fani ya uigizaji wa filamu nchini, Elizabeth Michael Kimemeta, maarufu kama Lulu, anayekabiliwa na kesi ya mauaji ya aliyekuwa msanii maarufu wa kiume wa fani hiyo, Steven Kanumba, keshokutwa atapanda kizimbani tena wakati kesi hiyo itakapoanza kuunguruma.

Lulu ambaye yuko nje kwa dhamana anakabiliwa na kesi hiyo katika Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam, akidaiwa kumuua Kanumba bila kukusudia, kinyume cha Kifungu cha 195 cha Kanuni za Adhabu (PC), April 7, 2012, nyumbani kwa marehemu Kanumba, Sinza Vatican.

Kwa mujibu wa ratiba ya vikao vya Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam vya mashauri ya jinai, kesi hiyo itasikilizwa keshokutwa na Jaji Sam Rumanyika kuanzia keshokutwa, Alhamis Oktoba 19 hadi Jumatatu Oktoba 23, mwaka huu.

Wakati upande wa mashtaka (Jamhuri) ukidai kuwa Lulu alimuua Kanumba bila kukusudia, hata hivyo Lulu mwenyewe wakati wa usikilizwaji wa awali mahakamani ambapo alisomewa maelezo ya kesi hiyo alikana mashtaka hayo ya kuua bila kukusudia.

Hivyo kesi hiyo itakapoanza kusikilizwa kuanzia keshokutwa, upande wa mashtaka utakuwa na wajibu wa kuwaita mashahidi mahakamani kutoa ushahidi na hata vielelezo kuthibitisha kuwa msanii huyo alitenda kosa hilo.

Hata hivyo ikiwa mara hii atakiri kosa hilo, basi Jamhuri haitalazimika kuita mashahidi wake kuthibitisha kosa hilo bali mahakama itamtia hatiani tu kwa kukiri kwake na kisha kumhukumu adhabu ambayo itaona kuwa inafaa.

Mshtakiwa anayepatikana na hatia ya kosa la kuua bila kukusudia, adhabu ya juu huwa ni kifungo cha Maisha.

Kwa hiyo mahakama inaweza kumhukumu mshtakiwa kifungo cha maisha, miaka 20,  mitano, mwezi, siku, saa ama kumwachia huru kabisa.

Lulu alipandishwa kizimbani kwa mara ya kwanza April 10, 2012,  katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu na kusomewa shtaka la kumuua Kanumba, lakini hakutakiwa kujibu chochote kwa kuwa mahakama hiyo haina mamlaka ya kisheria kusikiliza kesi za namna  hiyo, isipokuwa Mahakama Kuu.

Februari 17 msanii huyo alipandishwa kizimbani Mahakama Kuu na kujibu mashtaka hayo kwa mara ya kwanza, wakati wa usikilizwaji wa awali wa kesi hiyo (PH), ambapo alisomewa maelezo yote ya kesi inayomkabli.

Siku hiyo  Lulu  alikubali kuwa alikuwa na uhusiano wa kimapenzi na Kanumba, jambo ambalo ni miongoni mwa mambo manane ambayo aliyakiri mahakamani hapo, kama mambo yasiyobishaniwa katika kesi hiyo, lakini akakana kumuua Kanumba bila kukusudia.

Mambo mengine ambayo Lulu aliyakiri mahakamani hapo yaliyoko katika maelezo ya kesi hiyo ni pamoja na jina na anuani yake, kwenda nyumbani kwa Kanumba usiku wa tukio hilo, kuwa na ugomvi na Kanumba pia Kanumba kumzuia kutoka nje ya chumba alipojaribu kutoka ili akimbie.

Mengine ni kufanikiwa kutoka nje ya chumba cha marehemu Kanumba, kumweleza mdogo wa Kanumba (Seth Bosco) kuwa Kanumba ameanguka, kukamatwa kwake na polisi eneo la Bamaga, saa 11 Alfajiri ya usiku wa tukio hilo na kushtakiwa kwa kosa la kumuua Kanumba bila kukusudia.

Baada ya Lulu kukana mashtaka, Wakili wa Serikali, Monica Mbogo aliiarifu mahakama kuwa wakati wa usikilizwaji wa shauri hilo, upande wa mashtaka utakuwa na mashahidi wanne.

Aliwataja mashahidi hao kuwa ni pamoja na Seth Bosco, Daktari binafsi aliyekuwa akimhudumia Kanumba, Dk Paplas Kageiya, Ester Zephania na Askari D/Sgt Ernatus wa Kituo cha Polisi Oysterbay.

Pia Wakili Mbogo aliwasilisha mahakamani vielelezo viwili vitakayotumika kama sehemu ya ushahidi katika kesi hiyo ambayo ni taarifa ya kitabibu ya uchunguzi wa chanzo cha kifo cha Kanumba na ramani ya eneo la tukio.

Lulu kwa upande wake, mawakili wake Peter Kibatala na Fulgence Massawe waliiarifu Mahakama kuwa wakati wa usikilizwaji wa kesi hiyo kwenye utetezi watakuwa na mashahidi watano na vielelezo viwili. Hata hivyo hawakutaja majina ya mashahidi hao.

Share:

Nassari Apeleka Ushahidi wa Tatu TAKUKURU

Nassari Apeleka Ushahidi wa Tatu TAKUKURU

Mbunge wa Arumeru Mashariki, Joshua Nassari (Chadema)  amewasilisha ushahidi mwingine kwa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) kuhusu tuhuma za ununuzi wa madiwani wa Chama hicho.

Madiwani hao nane wa Chadema wamejiuzulu kwa kile walichoeleza kumuunga mkono Rais John Magufuli  jambo ambalo Nassari anadai siyo kweli bali walinunuliwa.

Akizungumza na waandishi wa habari jana nje ya ofisi ya Takukuru Upanga jiji ni humo alisema, " huu ni ushahidi wa tatu na kadri upepelezi ukiwa unaendelea nitaleta mwingine, hii ni kama filamu ya Isidingo."

Nassari alisema alitarajia Rais John Magufuli angewachukulia hatua wateule wake wanaohusishwa katika sakata hilo ili kupisha uchunguzi uweze kufanyika kwa uhuru.

"Tunajiuliza kwa nini Rais hawachukulii hatua DED, DAS au DC wote wa Arumeru kwa kutuhumiwa, watupeleke mahakamani na tungeomba suala hili lichukuliwe kwa uzito wake," alisema Nassari

Naye Mbunge wa Ubungo,  Saed Kubunea aliyeongozana na Nassari alisema,"Mimi nimeshiriki hususani kihabari kwani nimewashauri hawa kuutoa kwa umma ili jamii ijue ukweli."

"Tunachojiuliza kwa nini rais yupo kimya, kwa nini mawaziri na viongozi waliotuhumiwa Katika sakata la Almas na Tanzanite aliwasimamisha kwa nini hawa hataki," amehoji Kubenea
Share:

Mbowe kuzungumzia afya ya Lissu, michango

Mbowe kuzungumzia afya ya Lissu, michango

Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe leo atazungumzia kinachoendea katika hospitali ya Narobi nchini Kenya kuhusu afya ya Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano cha chama hicho, Tumaini Makene, Mbowe atazungumzia hayo leo katika ofisi za makao makuu ya chama hicho, Kinondoni jijini Dar es Salaam.

Pamoja na mambo mengine, Mbowe anatarajia kuzungumzia michango iliyokusanywa na matumizi yake.

“Kupitia kwa Mwenyekiti Freeman Mbowe, chama kitatoa taarifa kuhusu maendeleo ya Tundu Lissu, mrejesho wa michango na gharama za matibabu,” imeeleza taarifa hiyo na kuongeza kuwa mkutano huo utafanyika majira ya saa tano asubuhi.

Lissu anaendelea kupatiwa matibabu katika hospitali ya Nairobi nchini Kenya kutokana na majeraha aliyoyapata kwa kushambuliwa na risasi akiwa ndani ya gari, nyumbani kwake eneo la Area D mjini Dodoma.

Jana, Mbunge wa Singida Kaskazini, Lazaro Nyalandu aliwaambia watanzania kupitia Instagram kuwa alimtembelea Lissu na kuliona tabasamu lake, hivyo akawasihi waendelee kumuombea.
Share:

Diana Rwigara Amtaka Rais Kagame Amwachie Huru yeye na Familia Yake

Diana Rwigara Amtaka Rais Kagame Amwachie Huru yeye na Familia Yake

Kiongozi wa upinzani nchini Rwanda, Diane Rwigara amemtaka Rais Paul Kagame kumfutia mashtaka na kuwaachilia ndugu zake ambao wanashikili na jeshi la polisi nchini humo.

Rwigara amesema kuwa serikali imefanya jaribio la kuinyamazisha familia yake pamoja na wafuasi wake tangu alipotangaza kuwania nafasi ya uraisi katika uchaguzi uliofanyika mwezi Mei mwaka huu.

Aidha, ndugu hao watatu ambao walikamatwa mwezi uliopita, wameshtakiwa kwa makosa ya udanganyifu na uchochezi, tuhuma ambazo wameziita zenye mrengo wa kisiasa.

Hata hivyo,Rwigara alizuiliwa kuendelea na nia yake ya kuwania nafasi ya urais wa Rwanda, Uchaguzi ambao Kagame alishinda kwa kishindo kwa karibu asilimia tisini na tisa ya kura zote zilizopigwa

Share:

ACT- Wazalendo Kuuijadili Barua ya Mwigamba Kujitoa Ijumaa hii

ACT- Wazalendo Kuuijadili Barua ya Mwigamba Kujitoa Ijumaa hii

Chama cha ACT- Wazalendo kitakutana Ijumaa Oktoba 20, 2017 kujadili masuala kadhaa, likiwemo la kujizulu kwa mwenyekiti wake wa Kamati ya Kampeni na Uchaguzi Taifa na Mjumbe wa Kamati Kuu, Samson Mwigamba.

Mwigamba jana Jumatatu, Oktoba 16 aliandika barua ya kujizulu uongozi na kueleza atabaki kuwa mwanachama wa kawaida ili aweze kupata fursa ya kuwahoji kwa matendo viongozi.

"Nimeamua kukaa kando kwa kuwa tumekuwa hatukubaliani na baadhi ya mambo ndani ya chama na hasa kiongozi wetu… wacha nikae pembeni niwe mwanachama ili niwe na nafasi ya kuwahoji vizuri viongozi wetu masuala mbalimbali na nitabaki kuwa mwanachama mwema,’’ alisema .

Akizungumzia uamuzi huo, Kiongozi wa chama hicho, Zitto Kabwe amesema, “Nimepokea barua yake. Tutatafakari suala hilo na masuala mengine yanayohusiana na hayo kwenye kikao cha Kamati ya Uongozi wa chama Ijumaa.”

“Ndugu Mwigamba ataalikwa kwenye kikao hicho. Ninamshukuru sana kwa utumishi wake uliotukuka kwenye chama na ninamtakia kila la kheri. Mchango wake na kujitoa kwake kwa hali na mali hakutasahaulika kwenye chama chetu,” amesema  Zitto.

Share:

NEC: Waliopoteza vitambulisho ruksa kupiga kura uchaguzi mdogo wa madiwani

NEC: Waliopoteza vitambulisho ruksa kupiga kura uchaguzi mdogo wa madiwani

Wapiga kura waliopoteza vitambulisho vya kupigia kura watapata fursa ya kupiga kura katika uchaguzi mdogo wa madiwani wa kata 43 unaotarajiwa kufanyika Novemba 26, mwaka huu.

Hayo yamesemwa jana Jumatatu Oktoba 16, 2017 na Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), Ramadhani Kailima mjini Dodoma ikiwa ni siku ya pili ya mafunzo ya siku tatu kwa wasimamizi na wasimamizi wasaidizi wa uchaguzi yanayoratibiwa na kuendeshwa na NEC.

Kailima alisema wapiga kura hao wataruhusiwa kutumia vitambulisho vya uraia vinavyotolewa na Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (Nida), hati ya kusafiria na leseni ya udereva.

“Tume ya Taifa ya Uchaguzi kwa kuzingatia kifungu namba 62 (a) cha Sheria ya Uchaguzi wa Serikali za Mitaa, ambacho kinasema mpiga kura aliyeandikishwa kwenye daftari atakwenda mwenyewe kwenye kata aliyojiandikisha, kwenye kituo alichopangiwa, kumridhisha msimamizi wa kituo au msimamizi msaidizi wa uchaguzi kwamba yeye ndiye mpiga kura kwa kumuonyesha kadi ya kupigia kura lakini kinasema kwamba Tume inaweza ikaelekeza utambulisho mwingine wowote utakaomsaidia mpiga kura kuweza kupiga kura iwapo kadi hana,” alisema Kailima.

Mkurugenzi huyo wa uchaguzi alisema, “Tume kwa kuzingatia kifungu hicho, kuanzia uchaguzi huu imetoa maelekezo kwenye mafunzo haya kwamba Tume imekubali vitambulisho vifuatavyo vitumike, moja ni pasi ya kusafiria, pili ni kitambulisho cha Taifa kilichotolewa na Nida na mwisho ni leseni ya udereva.”

Alisema ruhusa hiyo imetolewa kwa sharti kwamba, “Majina na herufi yaliyopo kwenye kitambulisho hicho yafanane na majina na herufi zilizopo kwenye Daftari la Kudumu la Wapiga Kura.”

Kailima amesema NEC itakutana na vyama vya siasa hivi karibuni kuwajulisha juu ya maagizo hayo, lakini akasisitiza kwamba tofauti yoyote itakayokuwepo kwenye majina itamnyima mpiga kura fursa ya kupiga kura.

Alisema uamuzi huo umefikiwa kutokana na kuwepo kwa changamoto kubwa kwenye Daftari la Kudumu la Wapiga Kura ambalo kwa mara ya mwisho liliboreshwa mwaka 2015.
Share:

Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Alhamii ya Octoba 12

Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Alhamii ya Octoba 12



Share:

Categories

Ordered List

  1. Lorem ipsum dolor sit amet, consectetuer adipiscing elit.
  2. Aliquam tincidunt mauris eu risus.
  3. Vestibulum auctor dapibus neque.

Sample Text

Lorem ipsum dolor sit amet, consectetur adipisicing elit, sed do eiusmod tempor incididunt ut labore et dolore magna aliqua. Ut enim ad minim veniam, quis nostrud exercitation test link ullamco laboris nisi ut aliquip ex ea commodo consequat.

Definition List

Definition list
Consectetur adipisicing elit, sed do eiusmod tempor incididunt ut labore et dolore magna aliqua.
Lorem ipsum dolor sit amet
Consectetur adipisicing elit, sed do eiusmod tempor incididunt ut labore et dolore magna aliqua.

Support

Need our help to upload or customize this blogger template? Contact me with details about the theme customization you need.

Pages