Nassari Apeleka Ushahidi wa Tatu TAKUKURU
Mbunge wa Arumeru Mashariki, Joshua Nassari (Chadema) amewasilisha ushahidi mwingine kwa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) kuhusu tuhuma za ununuzi wa madiwani wa Chama hicho.
Madiwani hao nane wa Chadema wamejiuzulu kwa kile walichoeleza kumuunga mkono Rais John Magufuli jambo ambalo Nassari anadai siyo kweli bali walinunuliwa.
Akizungumza na waandishi wa habari jana nje ya ofisi ya Takukuru Upanga jiji ni humo alisema, " huu ni ushahidi wa tatu na kadri upepelezi ukiwa unaendelea nitaleta mwingine, hii ni kama filamu ya Isidingo."
Nassari alisema alitarajia Rais John Magufuli angewachukulia hatua wateule wake wanaohusishwa katika sakata hilo ili kupisha uchunguzi uweze kufanyika kwa uhuru.
"Tunajiuliza kwa nini Rais hawachukulii hatua DED, DAS au DC wote wa Arumeru kwa kutuhumiwa, watupeleke mahakamani na tungeomba suala hili lichukuliwe kwa uzito wake," alisema Nassari
Naye Mbunge wa Ubungo, Saed Kubunea aliyeongozana na Nassari alisema,"Mimi nimeshiriki hususani kihabari kwani nimewashauri hawa kuutoa kwa umma ili jamii ijue ukweli."
"Tunachojiuliza kwa nini rais yupo kimya, kwa nini mawaziri na viongozi waliotuhumiwa Katika sakata la Almas na Tanzanite aliwasimamisha kwa nini hawa hataki," amehoji Kubenea
No comments:
Post a Comment