Joshua Nassari Apeleka vielelezo vingine Takukuru

Joshua Nassari Apeleka vielelezo vingine Takukuru

Mbunge wa Arumeru Mashariki, Joshua Nassari amewasilisha vielelezo vingine katika Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) ili kuthibitisha tuhuma za rushwa dhidi ya viongozi wa Serikali wanaodaiwa kuwanunua madiwani wa Chadema waliohamia CCM.

Nassari aliwasili katika ofisi hizo jana saa 7:57 mchana na kutoka saa 11:33 jioni.

Wakati Nassari akiendelea na mahojiano hayo, maofisa wa Takukuru waliwafukuza waandishi wa habari waliokuwa katika eneo hilo wakisubiri kufanya mahojiano na mbunge huyo.

Hata alipotoka alikuwa amesindikizwa na maofisa hao waliokuwa wakiwazuia waandishi ambao waliamua kumsubiri nje ya lango la ofisi hizo wasifanye mahojiano.

Mmoja wa maofisa hao alimsindikiza mbunge huyo hadi alipohakikisha ameingia ndani ya gari na kuondoka eneo hilo.

Nassari aliwataka waandishi wamfuate katika eneo jingine kwa ajili ya mahojiano.

Akieleza sababu za mahojiano yake kuchukua muda mrefu, Nassari alisema hilo limesababishwa na wingi na uzito wa vielelezo alivyokuwa navyo.

“Nimewasilisha vielelezo na nimefungua jalada, nikatoa maelezo yangu mengine nimewaachia wao waendelee na uchunguzi.

“Ushahidi nilionao ni mkubwa mno umehusisha viongozi wengi, nami nimetoa kila nilichonacho na kuna nyaraka nyingine zipo Arusha zikifika kwa wakati muafaka nitaziwasilisha,” alisema.

Share:

No comments:

Post a Comment

Categories

Ordered List

  1. Lorem ipsum dolor sit amet, consectetuer adipiscing elit.
  2. Aliquam tincidunt mauris eu risus.
  3. Vestibulum auctor dapibus neque.

Sample Text

Lorem ipsum dolor sit amet, consectetur adipisicing elit, sed do eiusmod tempor incididunt ut labore et dolore magna aliqua. Ut enim ad minim veniam, quis nostrud exercitation test link ullamco laboris nisi ut aliquip ex ea commodo consequat.

Definition List

Definition list
Consectetur adipisicing elit, sed do eiusmod tempor incididunt ut labore et dolore magna aliqua.
Lorem ipsum dolor sit amet
Consectetur adipisicing elit, sed do eiusmod tempor incididunt ut labore et dolore magna aliqua.

Support

Need our help to upload or customize this blogger template? Contact me with details about the theme customization you need.

Pages