Msigwa: Iringa Tulitumia Vifaa vya Australia Kuwanasa Madiwani Wanaohongwa Wahamie CCM

Msigwa: Iringa Tulitumia Vifaa vya Australia Kuwanasa Madiwani Wanaohongwa Wahamie CCM

Mbunge wa Iringa Mjini kwa tiketi ya CHADEMA, Mchungaji Peter Msigwa amefunguka na kusema kuwa biashara ya kununua madiwani wa CHADEMA pia ilifanyika Iringa na kusema kuwa wao walitumia vifaa kutoka Australia kubaini hilo.

Peter Msigwa amesema hayo leo jijini Dar es Salaam baada ya kutoka Ofisi za Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) ambapo walikwenda kuwasilisha ushahidi wa Rushwa dhidi ya kununuliwa kwa madiwani hao na wateule wa Rais John Pombe Magufuli.

"Iringa mjini biashara nayo ilifanyika na nina ujasiri mkubwa kwamba muhusika mkuu wa biashara ya kununua madiwani Iringa Mjini ni ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkuu wa Wilaya pamoja na baadhi ya polisi.

"Hiyo mliona 'Episode' ya Arusha vilitumika vifaa vya Uingereza kule Iringa tulitumia vifaa vya Australia na sisi tutafungua jalada kama ambavyo Mkurugenzi wa TAKUKURU ametushauri kwa hiyo tusubiri sababu tumekabidhi kwenye korido za serikali na tunataka sheria zichukue mkondo wake huu uongo uongo wa kusema watu wanaunga mkono utendaji wa serikali tunataka ufike mwisho ili watu wakae kwenye nafasi zao kwa haki na jinsi ambavyo watu waliamua kuwachagua" alisema Msigwa
Share:

No comments:

Post a Comment

Categories

Ordered List

  1. Lorem ipsum dolor sit amet, consectetuer adipiscing elit.
  2. Aliquam tincidunt mauris eu risus.
  3. Vestibulum auctor dapibus neque.

Sample Text

Lorem ipsum dolor sit amet, consectetur adipisicing elit, sed do eiusmod tempor incididunt ut labore et dolore magna aliqua. Ut enim ad minim veniam, quis nostrud exercitation test link ullamco laboris nisi ut aliquip ex ea commodo consequat.

Definition List

Definition list
Consectetur adipisicing elit, sed do eiusmod tempor incididunt ut labore et dolore magna aliqua.
Lorem ipsum dolor sit amet
Consectetur adipisicing elit, sed do eiusmod tempor incididunt ut labore et dolore magna aliqua.

Support

Need our help to upload or customize this blogger template? Contact me with details about the theme customization you need.

Pages