Uhuru Kenyatta Amvaa Raila Odinga

Uhuru Kenyatta Amvaa Raila Odinga

Rais Uhuru Kenyatta amemjia juu Kiongozi wa NASA Raila Odinga baada ya kutangaza kutoshiriki uchaguzi wa marudio ambao unatarajiwa kufanyika Oktoba 26 mwaka huu nchini Kenya na kusema hata kama amejitoa Katiba ya Kenya haijazuia uchaguzi kutofanyika

Kenyatta amesema kuwa Odinga alitaka uchaguzi urudiwe jambo ambalo limeigharimu nchi ya Kenya fedha nyingi ambazo zingeweza kutumika kujenga barabara, zingeweza kutumika kujenga mahospitali na kutoa huduma mbalimbali kwa wananchi, lakini anashangaa mtu ambaye ametaka uchaguzi kurudiwa anajiengua tena.

"Rafiki yangu nasikia sasa umesema umejitoa baada ya kutupeleka peleka zaidi ya shilingi bilioni 12 hivi sasa zinatumika ili tufanye uchaguzi, pesa ambazo zingeweza kutumika kujenga barabara, zingetumika kujenga hospitali ya wananchi sasa zinatumika kwa uchaguzi ambao yeye ndiye aliitisha na sasa anasema hataki, kuna haki hapa jamanii, si mahakama ilisema IEBC haina makosa hayo masharti yote unatoa lakini tume hii si ndiyo imefanya viongozi hawa wengine wote kupatikana" alihoji Kenyatta

Mbali na hilo Kenyatta amesema kuwa wao wataendelea na mchakato wa uchaguzi kama kawaida na kusema huenda awepo au asiwepo Odinga uchaguzi utafanyika kama kawaida kama ambavyo tume ya uchaguzi ilitangaza.
Share:

No comments:

Post a Comment

Categories

Ordered List

  1. Lorem ipsum dolor sit amet, consectetuer adipiscing elit.
  2. Aliquam tincidunt mauris eu risus.
  3. Vestibulum auctor dapibus neque.

Sample Text

Lorem ipsum dolor sit amet, consectetur adipisicing elit, sed do eiusmod tempor incididunt ut labore et dolore magna aliqua. Ut enim ad minim veniam, quis nostrud exercitation test link ullamco laboris nisi ut aliquip ex ea commodo consequat.

Definition List

Definition list
Consectetur adipisicing elit, sed do eiusmod tempor incididunt ut labore et dolore magna aliqua.
Lorem ipsum dolor sit amet
Consectetur adipisicing elit, sed do eiusmod tempor incididunt ut labore et dolore magna aliqua.

Support

Need our help to upload or customize this blogger template? Contact me with details about the theme customization you need.

Pages