Abiria wa Bodaboda na Mmliki Kuwajibishwa
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mwigulu Nchemba amewataka abiria nchini kuendelea kutii sheria za usalama barabarani vinginevyo itaundwa sheria ambayo itawawajibisha.
Waziri ameyasema hayo jana mjini Moshi Mkoani Kilimanjaro kwenye uzinduzi wa wiki ya Usalama Barabarani ambapo aligusia usafiri wa pikipiki maarufu kama Bodaboda.
“Sheria itabidi imtambue mmiliki kwenye kosa la dereva pikipiki kukosa kofia ngumu (Helmet) ili wote wawajibishwe na hapo ndio wamiliki watakuwa makini kuhakikisha vyombo vyao vina kofia ngumu mbili, ya dereva na abiria”, alisema Mwigulu.
Aidha waziri Mwigulu aliongeza kuwa kutokana na takwimu za ajali za Bodaboda kuna haja ya kutumia taratibu ama sheria ambayo itamuwajibisha abiria endapo hatavaa kofia ngumu hali ambayo itasaidia abiria kudai kofia kabla ya kupanda Pikipiki.
Usafiri wa Bodaboda umekuwa na msaada mkubwa maeneo ya mijini na vijijini lakini umekuwa ukitajwa kama chanzo kikubwa cha ajali za barabarani kutokana na madereva wake kutofuata sheria za barabarani.
No comments:
Post a Comment