Jalada La Kesi La Mkurugenzi Wa Nida Liko Kwa DPP
Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jana imeelezwa kuwa jalada la kesi ya uhujumu uchumi dhidi ya aliyekiwa Mkurugenzi Mkuu Wa Vitambulisho vya Taifa (Nida), Dickson Maimu, lipo kwa DPP.
Mwendesha Mashtaka, wakili wa serikali, Peter Vitalis alieleza hayo mbelw ya Hakimu Mkazi Respicius Mwijage.
Alidai kuwa shauri hilo jana lilikuja kwa ajili ya kutajwa lakini jalada halisi la kesi hiyo liko kwa DPP na pia upelelezi bado haujakamilika, hivyo likirejeshwa ndipo itafahamika upelelezi umefikia wapi.
Hata hivyo, Hakimu Mwijage alisema kesi hiyo ina mwaka mmoja na upelelezi haujakamilika, hivyo wakamilishe ambapo ameahirishwa kesi hadi September 28/2017.
Katika kesi hiyo, mshtakiwa Maimu na wenzake, wanakabiliwana mashtaka ya 27 yakiwemo ya kutumia madaraka vibaya, kula njama, kutumia nyaraka za uongo kumdanganya mwajiri na kuisababishia Serikali hasara ya zaidi ya Sh 1,169,352,931.
Mbali ya Maimu, washtakiwa wengine Ni aliyekiwa Meneja Biashara Wa NIDA, Avelin Momburi, Mkurugenzi wa TEHEMA, Joseph Makani. Kaimu Mhasibu Mkuu wa NIDA, Benjamin Mwakatumbula, Mkurugenzi wa Kampuni ya Aste Insurance Brokers, Astery Ndege, Ofisa Usafirishaji, George Ntalima, Mkurugenzi wa Sheria, Sabina Raymond naXavery Kayombo.
No comments:
Post a Comment