Tundu Lissu Aikana Tweet ya Kumpongeza Ali Kiba na Kumponda Diamond

Tundu Lissu Aikana Tweet ya Kumpongeza Ali Kiba na Kumponda Diamond

Mwanasheria wa Chadema na Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu ameikana akaunti ya Twitter iliyoandika maoni kumpongeza mwanamuziki Alikiba, huku ikiwa na picha ya wanamuziki wanaofanya kazi chini ya lebo wa Wasafi.

Lissu amesema hafahamu chochote kuhusu akaunti hiyo na maoni yaliyotolewa akitaka mwandishi amfafanulie.

“Wananisingizia tu, ni wimbo gani wa Alikiba?” akimaanisha haelewi chochote kinachoendelea kuhusu uwepo wa wimbo wa “Seduce Me.”

Amesema akaunti hiyo si yake: “Hiyo akaunti ya Twitter si yangu na nilishasema tangu mwaka jana”

Jana Agosti 29, akaunti hiyo ilikuwa gumzo kwenye mitandao ikiwa imebeba ujumbe unaosema: “Hakuna kitu kibaya kama wanaume sita kuvaa mawigi kupambana na mtu mmoja. #seduceme#.

Tweet hiyo iliambatanishwa na picha ya Kundi la Wasafi wakiwa wamevaa mawigi ambayo waliitoa sambamba na wimbo wao wa“Zilipendwa”.

Mashabiki wanaomuunga mkono Alikiba walifurahi wakiamini kiongozi huyo amejiunga na wengine wengi ambao walijitokeza hadharani kumpongeza Alikiba.

Baadhi ya viongozi waliompongeza Alikiba ni Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk Hamis Kigwangalla; Mbunge wa Chalinze, Ridhiwani Kikwete; Mbunge wa Sengerema, William Ngeleja na Mbunge wa Viti Maalumu, Halima Bulembo.

Share:

No comments:

Post a Comment

Categories

Ordered List

  1. Lorem ipsum dolor sit amet, consectetuer adipiscing elit.
  2. Aliquam tincidunt mauris eu risus.
  3. Vestibulum auctor dapibus neque.

Sample Text

Lorem ipsum dolor sit amet, consectetur adipisicing elit, sed do eiusmod tempor incididunt ut labore et dolore magna aliqua. Ut enim ad minim veniam, quis nostrud exercitation test link ullamco laboris nisi ut aliquip ex ea commodo consequat.

Definition List

Definition list
Consectetur adipisicing elit, sed do eiusmod tempor incididunt ut labore et dolore magna aliqua.
Lorem ipsum dolor sit amet
Consectetur adipisicing elit, sed do eiusmod tempor incididunt ut labore et dolore magna aliqua.

Support

Need our help to upload or customize this blogger template? Contact me with details about the theme customization you need.

Pages