Mtoto Mchanga wa Miezi 6 Aliyejeruhiwa na Polisi Afariki Dunia
Mtoto wa miezi sita aliyejeruhiwa na maafisa wa polisi baada ya kutangazwa kwa matokeo ya uchaguzi yaliozua utata nchini Kenya amefariki, kulingana na familia yake.
Samantha Pendo alikuwa mahututi tangu siku ya Ijumaa baada ya kupata majeraha ya kichwa wakati polisi walipovamia nyumba yao katika mtaa wa mabanda magharibi mwa mji wa Kisumu.
Babake Joseph Abanja , ameliambia gazeti la Daily Nation: "Nataka haki kwa mwanangu,hakuwa akiandamana , babake hakuwa akiandamana pia.Mamake hakuwa akiandamana na badala yake walimuua.
''Nilifanya nilivyoambiwa kwenda kupiga kura na kurudi nyumbani'.Walitufuata hapa na kutupiga''.
Takriuban watu 24 waliuawa katika ghasia ambazo zilizuka baada ya uchaguzi wa tarehe 8 mwezi Agosti kulingana na shirika moja la haki za kibinaadamu
Kiongozi wa upinzani Raila Odinga alisema kuwa uchaguzi huo ulifanyiwa udanganyifu ili kumsaidia rais aliyepo madarakani Uhuru kenyatta kushinda.
Hatahivyo wachunguzi wa kimataifa wanasema kuwa uchaguzi huo ulikuwa huru na wa haki.
No comments:
Post a Comment