Jengo la Klabu ya Yanga Kupigwa Mnada Jumamosi Hii
Mkuu wa Kitengo cha Habari na Mawasiliano cha Klabu ya Simba SC, Haji Manara amefunguka na kuwapa pole watani wake wa jadi klabu ya Yanga kufuatia taarifa iliyotoka katika moja ya gazeti kuonyesha jengo lao litapigwa mnada Jumamosi ya wiki hii.
Haji Manara ametoa pole hiyo kupitia ukurasa wake wa Instgram na kuwaombea watani wao wajadi kwa kusema hivi sasa hali yao si nzuri hivyo kama jengo hilo litauzwa watakwenda kukaa wapi.
"Mungu wangu,Jumamosi hii jengo la Yanga linapigwa mnada, Wizara ya Ardhi waoneeni huruma kidogo wenzetu wana Swaumu kali, Daah!!sasa watahamia wapi? Shubamit" alimalizia Haji Manara
No comments:
Post a Comment