Julio arejeshwa kugombea TFF, Wanne waenguliwa kwa skendo ya Takukuru

WAKATI Kamati ya Uchaguzi ikimrejesha Jamhuri Kihwelo ‘Julio’ kwenye uchaguzi Mkuu wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) Agosti 12 mwaka huu mjini Dodoma, wagombea wengine wanne wameenguliwa.

Akizungumza na Waandishi wa Habari leo mjini Dar es Salaam, Mwenyekiti wa kamati hiyo, Wakili Revocatus Kuuli alisema kamati yake imewaondoa Shaffih Dauda, Elias Mwanjala, Benista Lugola na Ephraim Majige ambao walikuwa wanagombea ujumbe wa kamati ya utendaji.

“Tumejidhisha kuwa Julio ni kweli alisoma Kinondoni Muslim baada kupata vithibitisho kutoka baraza la mitihani lakini pia tumewaengua wagombea wanne ambao walikamatwa na TAKUKURU hivu karibuni kule Mwanza,” alisema Kuuli.

Pia Wakili Kuuli kamati yao imewaondoa wagombea hao lakini pia wana haki ya kukata rufaa kabla ya kamati yao kukaa Jumanne ya wiki ijayo kutoa orodha ya mwisho ya wagombea wote ili kuanza kampeni.

Jumla ya wagombea 74 walichukua fomu huku 58 wakiwania nafasi za ujumbe wa kamati ya utendaji katika Kanda mbalimbali hivyo kuondolewa wanne wanabaki 54 huku wagombea 10 wakiomba nafasi urais na makamu rais sita.

Share:

No comments:

Post a Comment

Categories

Ordered List

  1. Lorem ipsum dolor sit amet, consectetuer adipiscing elit.
  2. Aliquam tincidunt mauris eu risus.
  3. Vestibulum auctor dapibus neque.

Sample Text

Lorem ipsum dolor sit amet, consectetur adipisicing elit, sed do eiusmod tempor incididunt ut labore et dolore magna aliqua. Ut enim ad minim veniam, quis nostrud exercitation test link ullamco laboris nisi ut aliquip ex ea commodo consequat.

Definition List

Definition list
Consectetur adipisicing elit, sed do eiusmod tempor incididunt ut labore et dolore magna aliqua.
Lorem ipsum dolor sit amet
Consectetur adipisicing elit, sed do eiusmod tempor incididunt ut labore et dolore magna aliqua.

Support

Need our help to upload or customize this blogger template? Contact me with details about the theme customization you need.

Pages