Makamanda Zimamoto wapanguliwa

Makamanda Zimamoto wapanguliwa

Kamishna Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Tanzania Bara, Thobias Andengenye amefanya mabadiliko ya baadhi ya Makamanda wa Mikoa na Wakuu wa Vitengo wa Jeshi hilo.

Katika mabadiliko hayo, aliyekuwa Kamanda wa Zimamoto na Uokoaji Mkoa wa Arusha Kamishna Msaidizi (ACF), Bakari Mrisho amekuwa Mkuu wa Chuo na Mafunzo, nafasi yake inachukuliwa na Mrakibu (SF) Kennedy Komba, ambaye alikuwa Kamanda wa Zimamoto Mkoa wa Iringa na nafasi yake inachukiliwa na Mrakibu Msaidizi (ASF), James John toka Makao Makuu.

Kamanda wa Mkoa wa Kilimanjaro Kamishna Msaidizi (ACF), Gilbert Mvungi, amekuwa Kamanda wa Zimamoto Mkoa wa Kigoma, nafasi yake inachukuliwa na Kamishna Msaidizi (ACF), Baraza Mvano ambaye alikuwa Kamanda wa Zimamoto Mkoa wa Kigoma.

Kamanda wa Viwanja vya Ndege Nchini, Kamishna Msaidizi (ACF), Juma Kwiyamba amehamishiwa Makao Makuu, nafasi yake inachukuliwa na Kamishna Msaidizi (ACF) Christom Manyologa.

Kamishna Msaidizi (ACF) Fikiri Salla amekuwa Kamanda wa Mkoa wa Mbeya, anajaza nafasi iliyokuwa wazi baada ya Kamanda wa Zimamoto Mkoa wa Mbeya kuteuliwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama, Dkt. John Pombe Magufuli kuwa Kamishna wa Usalama dhidi ya Moto.

Kamanda wa Zimamoto Mkoa wa Pwani, Mratibu Msaidizi (ASF) Goodluck Zelote amekuwa Kamanda wa Zimamoto Mkoa wa Tanga, nafasi yake inachukuliwa na Mrakibu Msaidizi (ASF) Happy Shirima toka Makao Makuu.

Mratibu Msaidizi (ASF), Fatma Ngenya amekuwa Kamanda wa Zimamoto Mkoa wa Manyara, anachukua nafasi ya Mkaguzi Msaidizi (A/INSP) Heriel Kimaro ambaye amehamishiwa Makao Makuu.

Uhamisho huo ni Mabadiliko ya kawaida yanayotokea ndani ya Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, katika kuongeza ufanisi wa utendaji kazi.

Share:

No comments:

Post a Comment

Categories

Ordered List

  1. Lorem ipsum dolor sit amet, consectetuer adipiscing elit.
  2. Aliquam tincidunt mauris eu risus.
  3. Vestibulum auctor dapibus neque.

Sample Text

Lorem ipsum dolor sit amet, consectetur adipisicing elit, sed do eiusmod tempor incididunt ut labore et dolore magna aliqua. Ut enim ad minim veniam, quis nostrud exercitation test link ullamco laboris nisi ut aliquip ex ea commodo consequat.

Definition List

Definition list
Consectetur adipisicing elit, sed do eiusmod tempor incididunt ut labore et dolore magna aliqua.
Lorem ipsum dolor sit amet
Consectetur adipisicing elit, sed do eiusmod tempor incididunt ut labore et dolore magna aliqua.

Support

Need our help to upload or customize this blogger template? Contact me with details about the theme customization you need.

Pages