Zitto Kabwe Ahoji Ndege Mpya Zilizoahidiwa na Serikali Kwamba Zingekuja Mwez wa 7 Ziko Wapi?

Zitto Kabwe Ahoji Ndege Mpya Zilizoahidiwa na Serikali Kwamba Zingekuja Mwez wa 7 Ziko Wapi?

Ahadi ya Serikali ya kununua ndege ya tatu ambayo ilitakiwa kufika nchini Julai, imeshindwa kutekelezwa hadi sasa na Mbunge wa Kigoma Mjini, Zitto Kabwe amehoji kulikoni.

Mwaka jana, Serikali ilinunua ndege mbili aina ya bombadier na kuzikabidhi kwa Shirika la Ndege la Tanzania (ATCL) kwa ajili ya uendeshaji.

Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa na Naibu wake, Mhandisi Edwin Ngonyani kwa nyakati tofauti walikaririwa wakisema ndege hiyo itawasili Julai na kufanya idadi ya ndege za ATCL kuwa nne.

Hata hivyo, Mbunge wa Kigoma Mjini, Zitto Kabwe katika ukurasa wake wa Twitter jana alimuliza Profesa Mbarawa kuhusu ndege hiyo.

“Serikali iliahidi bungeni kuwa Julai 2017 mtapokea ndege nyingine ya Bombadier, leo ni Agosti iko wapi, lini itafika, nini kimetokea,”aliuliza Zitto

Profesa Mbarawa alimjibu kuwa “ni kweli kabisa ahadi ilikuwa Julai kuna taratibu za mwisho zinafanywa kabla ya kuwasili hivyo itawasili tu.”

Baada ya majibu hayo, Zitto alitaka kufahamu kutoka kwa Profesa Mbarawa ni lini ndege hiyo itawasili.

“Sababu za kuchelewa ni nini, delay (kuchelewa) ya mwezi mzima siyo dalili nzuri ndugu waziri, ni kwa sababu hamjalipa au zimezuiwa na wanaotudai,” aliuliza Zitto.

==>Angalia tweet zao hapo chini


Share:

No comments:

Post a Comment

Categories

Ordered List

  1. Lorem ipsum dolor sit amet, consectetuer adipiscing elit.
  2. Aliquam tincidunt mauris eu risus.
  3. Vestibulum auctor dapibus neque.

Sample Text

Lorem ipsum dolor sit amet, consectetur adipisicing elit, sed do eiusmod tempor incididunt ut labore et dolore magna aliqua. Ut enim ad minim veniam, quis nostrud exercitation test link ullamco laboris nisi ut aliquip ex ea commodo consequat.

Definition List

Definition list
Consectetur adipisicing elit, sed do eiusmod tempor incididunt ut labore et dolore magna aliqua.
Lorem ipsum dolor sit amet
Consectetur adipisicing elit, sed do eiusmod tempor incididunt ut labore et dolore magna aliqua.

Support

Need our help to upload or customize this blogger template? Contact me with details about the theme customization you need.

Pages