Diamond naye ajikuta mikononi mwa polisi
Mwanamuziki Diamond Platnumz jana ameripoti Kituo Kikuu cha Polisi cha Usalama Barabarani baada ya video yake kusambaa kwenye mitandao ya kijamii ikimuonyesha akiendesha gari bila kufunga mkanda huku akiachia usukani na kucheza ndani ya gari.
Daimond ambaye alikuwa ndani ya gari hilo pamoja na mpenzi wake, Zarinah Hassan, mama yake mzazi na mtoto wake walikuwa wakicheza wimbo mpya wa Diamond, Marry You aliomshirikika Ne-Yo.
Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Diamond ameweka picha akiwa na Kiongozi wa Kikosi cha Usalama Barabara, Kamanda Mpinga ambapo amewataka vijana wenzake kuhakikisha wanachukua tahadhari pindi wanapoendesha magari na kutumia barabara. Lakini pia ameeleza kuwa amelipa faini kwa mujibu wa sheria kutokana na kukiuka sheria za usalama barabarani.
“Leo nilireport kituo kikuu cha polisi wa usalama barabarani kutokana na Vidoe Clip tuliyopost naendesha gari barabarani bila kufunga mkanda na pia kuachia usukani na kucheza…. Nikapewa Onyo na Kulipa faini kulingana ya Mujibu wa sheria… tafadhali watanzania na Vijana wenzangu… tuhakikishe tunafunga mikanda pindi tupandapo na tuendeshapo Magari Maana ni Hatari kwa Maisha yetu na inaweza kukupeleka kunyea debe pia…🙏” ameandika Diamond
No comments:
Post a Comment