Jalada La Masogange Lakwama Kwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG)

Jalada La Masogange Lakwama Kwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG)

Msanii  maarufu anayepamba  video za wasanii wa muziki wa bongo Fleva (Video Queen) Agnes Gerald maarufu Masogange ameendelea kusota rumande, huku jalada lake likiendelea kuwa mikononi mwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG).

Masogange (25), alikamatwa na Jeshi la Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam kwa tuhuma za kujihusisha na uuzaji, usafirisha na kutumia dawa za kulevya.

Masogange alitarajiwa kupandishwa kizimbani Ijumaa wiki iliyopita lakini ilishindikana kutokana na majibu ya Mkemia Mkuu wa Serikali dhidi ya vipimo vyake kuonesha kama anatumia au hatumii dawa hizo kutokamilika.

Hata hivyo alitarajiwa kufikishwa tena Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu juzi ambapo alikwama tena kutokana na jalada lake kupelekwa kwa AG.

Wakili wa Masogange, Nick Kitege  amesema bado jalada la Masogange lipo kwa AG na anaendelea kulifanyia kazi na pindi litakapokamilika muda wowote anaweza kupelekwa mahakamani.

Alisema jalada hilo limechelewa kutokana na taratibu za kisheria zinazofanywa ili kukamilisha uchunguzi.

 “Bado tupo tunafuatilia na jalada la kesi yake kwa sasa lipo kwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali pindi taratibu zitakapokamilika atafikishwa mahakamani kati ya leo au kesho.

“Kuhusu ucheleweshwaji wa kesi hiyo ni kutokana na taratibu za kisheria, hivyo  Polisi waachwe wafanye kazi yao na sisi tunaangalia hatua zinazoendelea.

“Unajua hivi ni vyombo vya sheria na wanafanya kazi yao, wanahitaji muda kuchunguza na kutoa hoja zilizojitosheleza, bado wanahangaika kushughulikia suala hilo naamini leo tutapata jibu kamili,” alisema Kitege.

Julai mwaka 2013 Masogange alikamatwa Afrika Kusini katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Oliver Tambo, akiwa na mwenzake aliyejulikana kwa jina la Melisa Edward wakiwa na mzigo wa dawa za kulevya wenye thamani ya zaidi ya Sh bilioni 6.8.
Share:

No comments:

Post a Comment

Categories

Ordered List

  1. Lorem ipsum dolor sit amet, consectetuer adipiscing elit.
  2. Aliquam tincidunt mauris eu risus.
  3. Vestibulum auctor dapibus neque.

Sample Text

Lorem ipsum dolor sit amet, consectetur adipisicing elit, sed do eiusmod tempor incididunt ut labore et dolore magna aliqua. Ut enim ad minim veniam, quis nostrud exercitation test link ullamco laboris nisi ut aliquip ex ea commodo consequat.

Definition List

Definition list
Consectetur adipisicing elit, sed do eiusmod tempor incididunt ut labore et dolore magna aliqua.
Lorem ipsum dolor sit amet
Consectetur adipisicing elit, sed do eiusmod tempor incididunt ut labore et dolore magna aliqua.

Support

Need our help to upload or customize this blogger template? Contact me with details about the theme customization you need.

Pages