Kamanda Sirro Asimulia Anavyosumbuliwa na Wanawake Usiku
Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam Kamishna, Simon Sirro amesema miongoni mwa changamoto anazokutana nazo ni pamoja kupigiwa simu za vishawishi na wanawake hasa usiku wa manane, wakidhani anapata pesa nyingi kwenye kazi yake.
Kamishna Sirro amefichua siri hiyo hivi karibuni akiwa kwenye kipindi cha East Africa Breakfast, ambapo amesema pamoja na changamoto hizo, anajitahidi kukabiliana nazo kwa kuwa tayari amekwishawazoea.
Amesema kuwa kuna wanawake wengine wakiona amependeza kwenye tukio fulani, wanajua lazima atakuwa na pesa za kuwasaidia katika maisha yao hivyo wakati mwingine humpigia simu usiku, na yeye akidhani kuwa ni taarifa za uhalifu, lakini hukutana na vishawishi vikiambatana na sifa kedekede.
“Mwigine anaweza kukupigia simu tu usiku, kama unavyojua hawa wadada wa mjini, wakiniona wanajua niko vizuri, mwingine anakupigia anakuambia mzee tulikuona umevaa kofia vizuri, mjini kuna namna nyingi ya kuishi”. Amesema Kamanda Sirro
Aidha, Sirro ametaja changamoto nyingine ambazo hukutana nazo kuwa ni pamoja na suala la askari wake kulalamikiwa jambo linaloonesha dhahiri kama kiongozi ameshindwa kuwasimamia vijana anaowaongoza na mara nyingi huwa anachukua hatua.
Hata hivyo, Lingine ni uhalifu kuzidi katika eneo fulani na hufanya wananchi kuwa na uoga, na kupoteza imani kwa Jeshi la Polisi jambo ambalo linamfanya yeye ajisikie vibaya zaidi kuliko hata wananchi, huku nyingine ikiwa ni viongozi wa mitaa kutowajibika katika kudhibiti uhalifu pamoja na kuletewa
No comments:
Post a Comment