Mbowe Kaachiwa Huru baada ya Kuhojiwa na Kupekuliwa Usiku
Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Freeman Mbowe ameachiwa saa saba na robo usiku wa kuamkia leo baada ya kuhojiwa na kupekuliwa na Jeshi la Polisi.
Mbowe alikamatwa jana Jumatatu jioni wakati akienda kujisalimisha polisi na kupekuliwa nyumbani kwake kabla ya kuhojiwa hadi alipoachiwa usiku wa manane.
Ofisa habari wa chama hicho, Tumaini Makene amethibitisha taarifa za kuachiwa mwanasiasa huyo kuwa ni za kweli.
Hata hivyo, taarifa iliyosambazwa na Naibu Katibu Mkuu wa Chadema, Salum Mwalimu kupitia mitandao ya kijamii imesema kuwa chama hicho kitatoa taarifa zaidi juu ya tukio hilo leo.
“Tunawashukuru wote kwa sala, maombi na subira na hivyo kuhitimisha salama saa kumi za mwenyekiti wetu kuwa chini ya Jeshi la Polisi katika Kituo Kikuu cha Polisi, Dar es Salaam,” Mwalimu amesema.
No comments:
Post a Comment