Waziri Nape: Nitajiuzulu Uwaziri Kama Itabainika Natoka Kimapenzi na Wema Sepetu

Waziri Nape: Nitajiuzulu Uwaziri Kama Itabainika Natoka Kimapenzi na Wema Sepetu

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye, amesema atajiuzulu uwaziri endapo mtu atampelekea ushahidi wa kuwa na uhusiano wa kimapenzi na msanii yeyote.

Kauli hiyo ya Nape inakuja ikiwa ni takriban wiki tatu tangu Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda, aseme watu wanaotetea wale aliowataja hadharani kwa kuhusika na dawa za kulevya wengine ni wapenzi wao.

“Wengine wanaumia tunagusa wapenzi wao, wawasaidie waache si kupiga kelele tu, ujumbe umefika,” alisema Makonda katika moja ya mikutano yake.

Ingawa katika mkutano huo Makonda hakumtaja mtu kwa jina, lakini aliitoa kauli hiyo siku chache baada ya Nape kupinga mfumo wake wa kutaja majina ya watu hadharani, hususani wasanii na kuwatuhumu kuhusika na dawa za kulevya.

Nape alisema kuwataja watu bila ushahidi ni kuwachafulia majina yao waliyoyatengeza kwa muda mrefu.

Mbali na Nape, Mbunge wa Geita Vijijini, Joseph Msukuma (CCM), alizungumza mara kadhaa bungeni akimpinga Makonda kwa mfumo wake aliokuwa akitumia, kutaja majina ya watu wanaojihusisha na dawa za kulevya.

Akizungumza katika kipindi cha Dakika 45 kinachorushwa na kituo cha luninga cha ITV juzi, Nape alieleza kushangazwa na kitendo cha kuhusishwa kuwa na mahusiano na wasanii.

“Ila kama mtu ana ushahidi alete hapa mezani aseme Nape hili unalofanya, unafanya kwa sababu una uhusiano, na mtu akileta najiuzulu uwaziri.

“Hii ni katika watu ambao wanakosa hoja halafu wanasingizia hoja ambazo hazina msingi, ningefurahi mtu akisema Nape hana sababu ya kutumia busara, twende na hoja hii nyingine ni upuuzi,” alisema Nape.

Akizungumzia kuhusu kutajwa kuhusishwa kuwa na mahusiano ya kimapenzi na msanii nyota wa filamu, Wema Sepetu, Nape alisema wasanii wengi ni wadogo zake akiwamo Wema.

“‘Majority’ ya wasanii hawa ni wadogo zangu. Wamezungumza habari ya Wema, sasa nieleze ukweli kwamba baba yake, mzee Sepetu (Isack) na baba yangu (Moses Nnauye) ni mtu na kaka yake, kwa hiyo Wema ni mdogo wangu sana sana.

“Mama yake anatoka Singida, mama yangu naye anatoka Singida, ni mtoto mdogo lakini mtu akiamua apoteze ‘direction’ (mwelekeo) ya mjadala anaweza kuja na hoja nyingi sana.

“Mimi nimeanza kufanya kazi na wasanii, nimefanya nao kazi kwa miaka 16, hii ya uwaziri imekuja juzi tu. Pia msisahau hawa wasanii tuliwatumia kwenye kampemi ya CCM, mimi ndiyo nilikuwa Katibu wa Uenezi wa CCM.

“Ukizungumza burudani, hamasa na ‘publicity’ mimi ndio nashughulika nayo, hivyo kuwaingiza wasanii kwenye kampeni haikuwa kazi rahisi, sasa nikiwa nao karibu dhambi inatoka wapi, maana ndio nilipewa dhamana ya kuwasaidia. Hizi hoja zingine ni za kijinga kabisa,” alisema Nape.

Pamoja na mambo mengine, Nape alisema utaratibu uliokuwa ukitumiwa na Makonda kwa kutaja majina ya watu hadharani una madhara makubwa kwani unajenga chuki katika jamii.

Nape ambaye pia ni mbunge wa Mtama mkoani Lindi, alisema hakuna mahali popote duniani vita ya dawa za kulevya ilishinda kwa kupiganwa hadharani.

 “Tutajenga chuki kubwa sana kwenye jamii kama tukianzisha utaratibu wa kila mtu anasimama anamtaja mtu hadharani, ukishamtaja anaandikwa kwenye mitandao.

“Nchi itaingia kwenye vurugu kubwa bila sababu na wale wenye chuki zao watapitia hapo kuanza kutajana majina, tukitajana majina hadharani, hii vita hakuna mahali walipigana hadharani wakashinda popote duniani, haipo,” alisema.

Aidha alisema watu wasihukumiwe bila kosa bali haki itendeke na sheria na taratibu zifuatwe.

“Namshukuru Rais (Dk. Magufuli) ametumia busara namna ya kuli-handle (kulishughulikia) hili suala, amemteua kamishna na amemkumbusha waziri mkuu kwamba yeye ndie mwenyekiti wa hii kamati na mawaziri wako ndio wajumbe, sasa ameweka vita hii katika chombo salama.

“Pia namshukuru kamishna mwenyewe kasema tusitaje majina hadharani, lakini tufuate sheria na akasema hakuna jiwe litabaki juu ya jiwe, tutahakikisha tunasimamia sheria,” alisema Nape.

Share:

No comments:

Post a Comment

Categories

Ordered List

  1. Lorem ipsum dolor sit amet, consectetuer adipiscing elit.
  2. Aliquam tincidunt mauris eu risus.
  3. Vestibulum auctor dapibus neque.

Sample Text

Lorem ipsum dolor sit amet, consectetur adipisicing elit, sed do eiusmod tempor incididunt ut labore et dolore magna aliqua. Ut enim ad minim veniam, quis nostrud exercitation test link ullamco laboris nisi ut aliquip ex ea commodo consequat.

Definition List

Definition list
Consectetur adipisicing elit, sed do eiusmod tempor incididunt ut labore et dolore magna aliqua.
Lorem ipsum dolor sit amet
Consectetur adipisicing elit, sed do eiusmod tempor incididunt ut labore et dolore magna aliqua.

Support

Need our help to upload or customize this blogger template? Contact me with details about the theme customization you need.

Pages