Zitto Kabwe Atoa Kauli Nzito Kuhusu Sakata la Godbless Lema....Ataka ofisi ya DPP iwajibishwe

Zitto Kabwe Atoa Kauli Nzito Kuhusu Sakata la Godbless Lema....Ataka ofisi ya DPP iwajibishwe

Kitendo cha Mbunge wa Arusha mjini kukaa rumande kwa zaidi ya miezi minne sasa pasipo kupatiwa dhamana kimemfanya Mbunge wa Kigoma Mjini Mh. Zitto Zuberi Kabwe kushindwa kuzuia hisia zake na kutaka Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali iwajibishwe

Katika mtandao wake wa kijamii Mh. Zitto amedai kuwa kitendo cha  Mbunge huyo ambaye ni muwakilishi wa wananchi kunyimwa dhamana  ni siasa za ukomoaji ambazo zinajenga chuki kwenye jamii na chuki huwa zinazaa visasi.

"Haitoshi majaji kukemea Ofisi ya DPP, Mfumo wetu lazima uweke uwezo wa waendesha mashtaka wa aina ya kesi ya Mbunge wa Arusha Mjini kuwajibishwa. Wanasheria tazameni namna ya kuwajibisha ofisi ya DPP kwa uonevu wa makusudi dhidi ya wananchi" Ameandika Zitto Kabwe

Hata hivyo kauli hiyo ya Zitto imekuja mapema jana baada ya  majaji watatu  kutoka mahakama ya rufaa kuitaka ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa serikali na DPP kuwa makini na kuwataka kuwashikilia watu kwa misingi ya kisheria na kuongeza kuwa haipendezi na haingii akilini mtu  kushikiliwa kwa miezi minne bila sababu kwa misingi ya kumnyima haki ya dhamana.

"Mnatufanya wanasheria wote hatuna akili na mnachafua mpaka  mahakama, kwa hali ya kawaida mtu mumshikilie kwa misingi ya kisheria, lakini katika kesi hii tumepitia jalada hatujaona kitu chochote cha kumshikilia Lema hadi leo na imetushtua sana".Alisema Jaji Stella Mugasha.
Share:

No comments:

Post a Comment

Categories

Ordered List

  1. Lorem ipsum dolor sit amet, consectetuer adipiscing elit.
  2. Aliquam tincidunt mauris eu risus.
  3. Vestibulum auctor dapibus neque.

Sample Text

Lorem ipsum dolor sit amet, consectetur adipisicing elit, sed do eiusmod tempor incididunt ut labore et dolore magna aliqua. Ut enim ad minim veniam, quis nostrud exercitation test link ullamco laboris nisi ut aliquip ex ea commodo consequat.

Definition List

Definition list
Consectetur adipisicing elit, sed do eiusmod tempor incididunt ut labore et dolore magna aliqua.
Lorem ipsum dolor sit amet
Consectetur adipisicing elit, sed do eiusmod tempor incididunt ut labore et dolore magna aliqua.

Support

Need our help to upload or customize this blogger template? Contact me with details about the theme customization you need.

Pages