Lusinde Amvaa Mbunge Mwenzake wa CCM Kwa Kugana Muda na Mbunge wa CHADEMA
Mbunge wa Mtera (CCM), Livingstone Lusinde amesema kitendo alichofanya Mbunge mwenzake wa Jimbo la Mara CCM, Boniface Getere cha kugawana muda na mbunge wa Serengeti (Chadema), Marwa Ryoba ni utovu mkubwa wa nidhamu.
Lusinde ni mmoja wa wabunge wa CCM waliomlalamikia Getere kumpa dakika tano Ryoba ili aweze kuchangia taarifa za kamati za Bunge Kamati ya Ardhi, Maliasili na Utalii na ya Kilimo, Mifugo na Maji baada ya mwenyekiti wa Bunge, Mussa Hassan Zungu kumruhusu azungumze kwa dakika kumi.
“Duniani kote kazi ya upinzani ni kuipinga Serikali iliyopo madarakani na kazi ya wabunge wa chama tawala ni kuishauri Serikali na kuipongeza pale inapofanya vizuri, hizi ni kambi mbili tofauti,huwezi kuwapa muda wapinzani” alisema Lusinde.
Mbunge wa Ubungo (Chadema), Saed Kubenea alisema haoni ubaya kwa mbunge wa CCM kumpa muda mbunge wa upinzani bali anachokiona CCM wanahamishia kampeni bungeni.
Hata hivyo, alipoulizwa Getere iwapo haoni kama amefanya makosa kumgawia mbunge wa upinzani, alisema hajaona madhara yoyote kwa kitendo chake hicho.
No comments:
Post a Comment