Mwanamke Atoa Tangazo Gazetini Baada ya Kugundua Mumewe Anachepuka Nje ya Ndoa
Mtandao wa TUKO umeripoti kuhusu huyu Mwanamke aliyewaaacha wengi na mshangao baada ya kutumia njia isiyo ya kawaida kumzuia mumewe kuchepuka na kuchukua Mwanamke mwingine.
Mwanamke huyo Mkenya aliyetambulika kwa jina la Wanjiru Kamami ama Shiro alichapisha tangazo kwenye gazeti moja la Kenya akitaka kujuzwa habari na yeyote atakayemwona mumewe akiwa na ‘mpango wa kando’ au Mchepuko.
Katika kitendo cha Mwanamke huyo kuonyesha kwamba yuko serious akaamua kuandika na jina la mume wake pamoja na namba ya simu kwenye hilo tangazo lililosomeka "Hii ni kuwajulisha kwamba huyu aliye kwenye picha ni Mume wa Wanjiru Kamami toka mwaka 1982
"Ukimuona anadanganya Wasichana wa shule, Wanawake wengine au kina mama wa sokoni, mwambie aende nyumbani kwa mke wake au piga simu au sms kwenye 0751 993 571"
No comments:
Post a Comment