Ridhiwani Kikwete Afafanua Sakata la Diamond Kupewa Bendera Ya Taifa
Mwimbaji Mtanzania Diamond Platnumz alikabidhiwa bendera ya taifa na Waziri wa michezo na sanaa Nape Nnauye baada ya kualikwa kutumbuiza kwenye ufunguzi wa michuano ya soka ya Afrika 2017 kwenye taifa la Gabon.
Baada ya hapo Ridhiwani aliandika kuhusu timu ya taifa ya soka ambapo wengine waliitafsiri post yake kama amechukia Diamond kupewa bendera lakini leo kupitia The Beauty TV amehojiwa na kutoa ufafanuzi.
"Kwanza watu wanatakiwa kuelewa kwamba ile post haikuwa kwasababu ya Diamond na hata ukisoma kwenye maandishi yangu hakuna sehemu Diamond ametajwa isipokua msg iliyo pale inaweza kuwa inamgusa Diamond.
"Kilichonifanya niandike ile msg ni ule wivu wa kuona kwamba mashindano yanayokwenda kufanyika ni ya mpira wa miguu, sisi tunayo timu ya taifa ya mpira wa miguu lakini kilichotushangaza badala ya kutoa bendera kwa timu ya mpira wa miguu tunawapa Waburudishaji kina Diamond
"Matarajio yetu sisi watu wa mpira ni kuona Nahodha wa timu ya taifa akipokea Bendera, aliyepaswa kupokea bendera ni captain wa timu ya taifa……. hii pia lakini ni kuwapa changamoto TFF, je wao wanashangilia kuona Diamond amepewa bendera?
"Mtazamo wangu mkubwa ulijikita huko na sio mtazamo wa kwamba Diamond sijui nani………. NO NO… Diamond yeye nampongeza sana kwa hatua aliyofika, anafanya kazi nzuri na ndio maana watu wamemuona wamempa nafasi ya kwenda kutumbuiza lakini kikubwa ni nini ajenda kubwa Gabon? ajenda ni mpira wa miguu.
"Diamond sio mcheza mpira wa miguu, hata kama anashabiki atakua ni mshabiki tu…. sisi kama Mashabiki wa soka tunaona wenzetu wanajiandaa kuhakikisha timu zao zinafuzu kwenda kucheza katika hatua ile, sisi kwetu tunaandaa Wanamuziki kwenda kuburudisha, ni jambo la kusikitisha sana"
No comments:
Post a Comment