Tundu Lissu akamatwa na polisi....Asafirishwa Usiku kutoka Dodoma hadi Dar
Mwanasheria Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Tundu Lissu amekamatwa na Jeshi la Polisi wakati akitoka bungeni mkoani Dodoma na kusafirishwa usiku kwenda Jijini Dar es salaam.
Lissu ambaye pia ni Mbunge wa Singida Mashariki(Chadema) na Mnazimu wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni ametiwa nguvuni kama ilivyokuwa kwa Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema.
Kamanda wa Mkoa wa Dodoma, Lazaro Mambosasa, amesema kuwa wamemkamata Tundu Lissu kutokana na makosa aliyoyafanya Dar es salaam.
”Sisi tunawajibu wa kumkamata na kumpeleka sehemu husika, tumemkamata kwa maagizo tuliyopewa kutoka Dar es salaam na kama unataka kujua muulize kamanda wa Dar es salaam,”alisema jana Kamanda Mambosasa.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo Freeman Mbowe, alisema kuwa hafahamu sababu za kukamatwa na kusafirishwa kwa Mwanasheria Mkuu wa chama hicho.
“Ni kweli wamemkamata lakini mpaka sasa hatujui lengo lake ni nini na wanampeleka wapi kwa ajili ya nini na kwa lengo lipi,”amesema Mbowe.
No comments:
Post a Comment