Zitto Kabwe: Sasa kukamata wabunge hovyo hovyo mwisho
Mbunge wa Kigoma mjini Zitto Kabwe amefunguka na kusema ile hali ya polisi kuwakamata wabunge hovyo sasa mwisho baada ya jana Ndugai kutoa uamuzi kuwa Afisa yoyote wa Serikali ambaye atakuwa akimuhitaji mbunge ni lazima kwanza atoe taarifa kwa spika
Hali hii imefikia baada ya Jumatano bunge kupitisha azimio la kutaka kwanza ruhusa ya spika wa bunge pale vyombo vya dola kama polisi wanapokuwa wanamuhitaji mbunge yoyote kwa jambo lolote.
"Leo (jana) Spika wa Bunge ametoa uamuzi wa Spika kwamba Afisa wa Serikali anapomtaka mbunge kwa jambo lolote lile lazima kwanza kupata kibali chake. Mabunge yote ya Jumuiya ya Madola hulinda kwa wivu mkubwa hadhi yake kama mhimili. Sasa kukamata kamata wabunge hovyo mwisho. Lazima mihimili iheshimiane. Sasa tuone kama Sirro atamfuata Mbunge wa Hai kama alivyosema" alisema Zitto Kabwe
Mbali na hilo Mhe. Zitto Kabwe ametoa pongezi kwa wabunge wote pamoja na Spika wa bunge kwa kuonyesha msimamo na kupigania heshima ya bunge
"Nawapongeza wabunge wote kwa kuonyesha msimamo katika jambo hili na ninampongeza sana Spika Ndugai kwa kusimamia heshima ya bunge lake" Alimalizia Zitto Kabwe
No comments:
Post a Comment