VIDEO: Kilichowapata abiria wa Kilimanjaro na Arusha leo Ubungo DSM
Kwenye msimu huu wa sikukuu hali ya usafiri wa mabasi kwenda mikoani huwa si ya kuridhisha kutokana na kuwepo kwa changamoto mbalimbali kupandishwa kwa nauli na kukosa usafiri kutokana na kuwepo kwa idadi kubwa ya abiria.
Kwa kuliona hilo jeshi la polisi kitengo cha usalama barabarani wakishirikiana na SUMATRAwalitoa vibali kwa mabasi aina ya Eicher na Coaster ambazo zilikuwa zikitumika kwa ajili ya usafiri wa daladala Dar es salaam ili kutoa huduma ya usafiri kwa maeneo ambayo yamekuwa na uhaba wa mabasi ambayo ni Arusha na Moshi.
Leo December 23 2016 Ayo TV na millardayo.com imeshuhudia magari hayo yakitoka kwenye stendi ya mabasi Ubungo yakiwa na abiria wa Moshi na Arusha, Licha ya kuwepo kwa mabasi hayo, Leo December 23 2016, AyoTV na millardayo.com imeshuhudia abiria wengi wakiwa wamekosa usafiri huku wengine wakilalamika kupandisjhiwa nauli.
Aidha AyoTV imezungumza na Mkurugenzi wa udhibiti wa usafiri wa barabara waSUMATRA Johansen Kahatano ambapo amesema wamewakamata baadhi ya mawakala wa mabasi hayo ambao wameongeza nauli kutoka iliyopangwa na SUMATRA Sh 23,000 mpaka kufika 35,000 kwa 45,000.
ULIKOSA HII YA JESHI LA POLISI LILIVYOTANGAZA MAGARI MAPYA YATAKAYORUHUSIWA KUBEBA ABIRIA, BONYEZA PLAY HAPA CHINI
Unazitaka Breaking NEWS na Stori zote? ungana na Millard Ayo kwenye Facebook Twitter Instagram na Youtube na atakuletea matukio yote ya picha, video na habari iwe usiku au mchana…. bonyezahapa >> FB https://web.facebook.com/mwamkili.gks
No comments:
Post a Comment