Penzi la Bibi wa Miaka 60 Laua Kijana wa Miaka 23

Penzi la Bibi wa Miaka 60 Laua Kijana wa Miaka 23

KIJANA mwenye umri wa 23 na mpenzi wake, bibi mwenye umri wa miaka 60 , wakazi wa kijiji cha Tentula, Kata ya Ikozi wilayani Sumbawanga, wanashikiliwa na polisi wakihutumiwa kumshambulia na kumuua kikatili jirani yao aitwae Desder Justino (23) kwa kile kinachoelezwa kuwa ni wivu wa mapenzi.

Inaelezwa kuwa, Justino pia alikuwa na mahusiano ya kimapenzi na bibi huyo.

Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Rukwa, George Kyando alithibitisha tukio hilo na kueleza kuwa mauaji hayo yalitokea Desemba 21 mwaka huu saa nne asubuhi katika nyumba ya mwanamke huyo iliyopo kijijini Tentula.

Taarifa kutoka kijijini humo zinadai kuwa, mwanamke huyo licha ya umri wake kuwa mkubwa, alikuwa na uhusiano wa kimapenzi na vijana hao wawili wa rika moja.

Kamanda Kyando hakuwa tayari kutaja majina ya wapenzi hao ambao ni watuhumiwa wa mauaji kwa sababu za uchunguzi.

Lakini alisema mwanaume ana umri wa miaka 23 huku mpenzi wake ana umri wa miaka 60. Akielezea zaidi, Kamanda Kyando alisema siku ya tukio Justino alikwenda nyumbani kwa mwanamke huyo ambaye anadaiwa kuwa na uhusiano naye wa kimapenzi na kumkuta kijana mwingine (mtuhumiwa), na hapo ndipo ugomvi ukaibuka baina ya vijana hao.Alisema Justino alijeruwa kichwani.

“Wawili hao yaani wapenzi hao (mwanamke na mwanaume) walimshambulia Justino (Desder) kwa kumpiga kichwani na kitu chenye ncha kali na kumjeruhi vibaya na alikufa akiwa anatibiwa hospitalini,” alisema Kamanda Kyando na kuongeza  kuwa, watuhumiwa hao wanashikiliwa na watafikishwa mahakamani uchunguzi wa awali utakapokamilika.

Share:

No comments:

Post a Comment

Categories

Ordered List

  1. Lorem ipsum dolor sit amet, consectetuer adipiscing elit.
  2. Aliquam tincidunt mauris eu risus.
  3. Vestibulum auctor dapibus neque.

Sample Text

Lorem ipsum dolor sit amet, consectetur adipisicing elit, sed do eiusmod tempor incididunt ut labore et dolore magna aliqua. Ut enim ad minim veniam, quis nostrud exercitation test link ullamco laboris nisi ut aliquip ex ea commodo consequat.

Definition List

Definition list
Consectetur adipisicing elit, sed do eiusmod tempor incididunt ut labore et dolore magna aliqua.
Lorem ipsum dolor sit amet
Consectetur adipisicing elit, sed do eiusmod tempor incididunt ut labore et dolore magna aliqua.

Support

Need our help to upload or customize this blogger template? Contact me with details about the theme customization you need.

Pages