Trump aitaka Marekani kuboresha silaha za nuklia
Donald Trump ameitaka Marekani kuboresha zaidi uwezo wake wa zana za nuklia.
Rais huyo mteule ambaye ataingia ofisini mwezi ujao amesema kuwa Marakani ni lazima ichukue hatua kama hizo, hadi wakati ulimwengu utatathmini suala la nuklia.
Trump aliyazungumza hayo saa kaadha baada ya rais wa Urusi Vladimir Putin kusema kuwa Urusi inahitaji kuboresha uwezo wake silaha za nuklia
Marekania ina silaha 7,100 za nuklia huku Urusi ikiwa inamiliki silaha 7,300 kulingana na shirika la kudhibithi silaha la marekani.
Trump aliyaandika hayo kwenye akaunti yake ya mtando wa twitter
Wakati wa kampeni, Trump alisema kuwa silaha la nuklia ndilo tatizo kubwa zaidi linaloikumba dunia.
Mgombea wa chama cha Democratic Hillary Clinton mara kwa mara alimtaja Trump kuwa mtu asiye na uvumilivu wa kuweza kuzuia vita vya kinuklia.
No comments:
Post a Comment