Mwandishi wa ITV Aliyekamatwa Kwa Amri ya Mkuu wa Wilaya Aachiwa Kwa Dhamana

Mwandishi wa ITV Aliyekamatwa Kwa Amri ya Mkuu wa Wilaya Aachiwa Kwa Dhamana

Mwandishi  wa kujitegemea wa kituo cha televisheni cha ITV, Halfani Lihundi ameachiwa kwa dhamana kutoka katika kituo cha Polisi cha Changamoto, Usa River wilayani Arumeru mkoani Arusha alikokuwa anashikiliwa tangu juzi, na kutakiwa kuripoti kituoni hapo Desemba 27, mwaka huu.

Alikuwa anashikiliwa kwa amri ya Mkuu wa Wilaya ya Arumeru, Alexander Mnyeti, baada ya kuripoti habari inayoelezwa na mkuu huyo wa wilaya kuwa haikuwa sawa na kuamuru kukamatwa kisha, kulala mahabusu na hatimaye kufanikiwa kutoka jana saa tisa alasiri.

Awali, waandishi wa habari wa Arusha walikusanyika kituoni hapo ili kujua hatma ya mwenzao na baadaye kuamua kwenda kumuona Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi ili kumweleza kuwa mwenzao amekamatwa kwa sababu ya migogoro ya wananchi.

Wakati Lukuvi anatoka kwenye kikao cha kujadili migogoro ya ardhi kilichofanyika ukumbi wa Mkuu wa Mkoa wa Arusha, waandishi waliimba wimbo wenye lengo la kufikisha ujumbe kuwa, wanataka wenzao aachiwe huru. Waliimba; “Solidarity Forever, Bring Back Halfani Lihundi.”

Lukuvi alisema hahusiki na suala hilo na kuwasihi wanahabari kwenda naye Usa River kwenye mkutano ambapo Mnyeti atatoa tamko juu ya suala hilo.

Lakini Mnyeti alipokuwa akitoka kikaoni hapo aliulizwa na waandishi kuhusu suala hilo na kosa lipi limefanya Lihundi kushikiliwa Polisi, lakini hakuzungumza chochote na kuelekea kwenye gari lake kusubiri msafara wa Lukuvi. 

Awali, ilidaiwa kuwa Mnyeti ndiye aliyeamuru Lihundi akamatwe kwa madai ya kuandika habari za uchochezi za kijiji cha Leguruki, Arumeru.

Alisema alipotaka kujua kosa analoshitakiwa nalo Lihundi, alijibiwa hana kosa ila yupo kwa amri ya Mkuu wa Wilaya. Hata hivyo, RB ya Polisi Usa River 4763/2016 inaonesha ana kosa la uchochezi.
Share:

1 comment:

Categories

Ordered List

  1. Lorem ipsum dolor sit amet, consectetuer adipiscing elit.
  2. Aliquam tincidunt mauris eu risus.
  3. Vestibulum auctor dapibus neque.

Sample Text

Lorem ipsum dolor sit amet, consectetur adipisicing elit, sed do eiusmod tempor incididunt ut labore et dolore magna aliqua. Ut enim ad minim veniam, quis nostrud exercitation test link ullamco laboris nisi ut aliquip ex ea commodo consequat.

Definition List

Definition list
Consectetur adipisicing elit, sed do eiusmod tempor incididunt ut labore et dolore magna aliqua.
Lorem ipsum dolor sit amet
Consectetur adipisicing elit, sed do eiusmod tempor incididunt ut labore et dolore magna aliqua.

Support

Need our help to upload or customize this blogger template? Contact me with details about the theme customization you need.

Pages