Senegal kuongoza "kupinduliwa kwa Jammeh"
Senegal itaongoza hatua za kijeshi kumuondoa madarakani rais wa Gambia Yahya Jammeh ikiwa atakataa kung'atuka wakati kipindi chake kitakapokamilika tarehe 19 mwezi Janauri kwa mujibu wa afisa wa cheo cha juu wa jumuiya ya Ecowas.
"Vikosi vya kijeshi viko tayari kuwapa watu matakwa yao, ikiwa wapatanishi wanaoongozwa na rais wa Nigeria Muhammadu Buhari watashindwa kumshawishi bwana Jammeh kuachia madaraka, alisema Marcel Alain de Souza.
- Jeshi ladhibiti jengo la tume ya uchaguzi Gambia
- Kiongozi wa upinzani ashinda uchaguzi wa urais Gambia
Ameongeza kuwa si matarajio ya Ecowas kuwasha moto eneo hilo na ikiwa bwana Jammeh anapednma watu wake, anahitaji kuondoka madarakani.
Awali Jammeh alikubali kushindwa na mfanyabiashara Adama Barrow wakati wa uchaguzi wa Disemba Mosi, lakini baadaye akaagiza kubadilishwa kwa matokeo akidai kuwa kulikuw na udanganyifu.
No comments:
Post a Comment