Mwanza Yatoa Msaada wa Chakula Kwa Kaya 231 Zilizoathiriwa na Mvua

Mwanza Yatoa Msaada wa Chakula Kwa Kaya 231 Zilizoathiriwa na Mvua

Serikali wilayani Nyamagana Mkoani Mwanza  imetoa msaada wa vyakula kwa watu ambao nyumba zao ziliezuliwa paa na mvua iliyonyesha wiki iliyopita iliyoambatana na upepo. Mvua hiyo iliathiri kaya 231 zenye watu 800 ambao mpaka sasa hawana makazi. 

 Vyakula vilivyogawiwa ni kilo 3,760 za unga na kilo 1,000 za maharagwe vyote vikiwa na thamani ya Sh7.3 milioni. 

Akizungumza baada ya kukabidhi vyakula hivyo kwa nyakati tofauti, mkuu wa Wilaya ya Nyamagana, Marry Tesha alisema msaada huo umetolewa na Serikali kwa kushirikiana na wadau wengine. 

Alisema vyakula katika Kata za Mahina waligawa kwa kaya (94), Butimba (64), Nyegezi (61) na Mkuyuni (12). Mkuu huyo wa wilaya aliwataka viongozi wa maeneo hayo kuhakikisha msaada huo unatumika kwa malengo yaliyokusudiwa.

Pia, alito wito kwa wananchi kujenga nyumba imara zinazoweza kuhimili mikikimikiki, kwa kuwa nyingi zilizobomoka, hazikuwa imara. 

Ally Juma, ofisa mtendaji wa Kata ya Mahina ambako nyumba za kaya 94 ziliezuliwa, alisema wamiliki wameshindwa kupaua upya kutokana na uduni wa kipato. 

 Ofisa Mtendaji Kata ya Nyegezi, Charles Musa alitoa wito kwa wananchi kupanda miti kwenye makazi yao ili kuepuka madhara yatokanayo na upepo mkali. 

Naye Amina Rashid, ambaye ni muathirika wa mvua hizo anayeishi Mahina, aliiomba Serikali iendelee kuwasaidia kwa sababu madhara waliyoyapata ni makubwa na uwezo wengi ni mdogo. 
Share:

No comments:

Post a Comment

Categories

Ordered List

  1. Lorem ipsum dolor sit amet, consectetuer adipiscing elit.
  2. Aliquam tincidunt mauris eu risus.
  3. Vestibulum auctor dapibus neque.

Sample Text

Lorem ipsum dolor sit amet, consectetur adipisicing elit, sed do eiusmod tempor incididunt ut labore et dolore magna aliqua. Ut enim ad minim veniam, quis nostrud exercitation test link ullamco laboris nisi ut aliquip ex ea commodo consequat.

Definition List

Definition list
Consectetur adipisicing elit, sed do eiusmod tempor incididunt ut labore et dolore magna aliqua.
Lorem ipsum dolor sit amet
Consectetur adipisicing elit, sed do eiusmod tempor incididunt ut labore et dolore magna aliqua.

Support

Need our help to upload or customize this blogger template? Contact me with details about the theme customization you need.

Pages