Rais Magufuli Amwapisha Jenerali Venance Mabeyo kuwa Mkuu mpya wa Majeshi ya Ulinzi
Rais John Magufuli leo amemuapisha Mkuu mpya wa Majeshi ya Ulinzi, Jenerali Venance Mabeyo Ikulu jijini Dar es Salaam.
Jenerali Mabeyo aliteuliwa na Rais Magufuli Alhamisi iliyopita kushika wadhifa huo baada ya Jenerali Devis Mwamunyange kustaafu.
Jenerali Mabeyo alikuwa Luteni Jenerali kabla ya kupandishwa cheo kuwa Jenerali.
Kabla ya kuapishwa Jenerali huyo, Rais John Magufuli alimvalisha Luteni Jenerali Venance Mabeyo cheo kipya na kuwa Jenerali.
Pia, Rais Magufuli amemuapisha Mnadhimu Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi nchini, Luteni Jenerali James Mwakibolwa akichukua nafasi iliyoachwa wazi na Jenerali Mabeyo.
No comments:
Post a Comment