Afande Sele aanika sababu za kuitosa ACT Wazalendo

Afande Sele aanika sababu za kuitosa ACT Wazalendo

Mwanamuziki mkongwe, Selemani Msindi maarufu kama Afande Sele ameeleza sababu zilizopelekea jana kutangaza kung’atuka ndani ya Chama Cha ACT – Wazalendo mwaka mmoja baada ya harakati za uchaguzi Mkuu ambao aliutumia kugombea ubunge wa Morogoro Mjini.

Afande Sele ameeleza kuwa moja kati ya sababu zilizopelekea yeye kung’atuka ni kutofikia malengo yake ya kuingia ndani ya chama hicho ya kupata ubunge.

“Nimejitoa ACT- Wazalendo kwa makusudi kabisa na hili lilikuwa ni jambo tarajiwa, kitu cha kwanza moja ya matarajio yalikuwa baada ya mimi kuingia ACT nakuwa Mbunge ila sasa sikupata Ubunge na kama ningeupata Ubunge basi nisingejitoa ndani ya chama,” Anasema Afande Sele .

Jana, kupitia ukurasa wake wa Facebook, mwanamuziki huyo alieleza kuwa amechukua uamuzi huo sio kwa bahati mbaya hivyo uamuzi wake uheshimiwe. Alisisitiza kuwa hatajiunga na chama chochote cha siasa hadi pale ambapo ataamua vinginevyo.

Mei mwaka jana, Afande Sele alitangaza kugombea ubunge wa Morogoro mjini kupitia ACT-Wazalendo lakini hakufanikiwa kuupata ubunge wa jimbo hilo kupitia sanduku la kura, Oktoba 25 mwaka jana.

Share:

No comments:

Post a Comment

Categories

Ordered List

  1. Lorem ipsum dolor sit amet, consectetuer adipiscing elit.
  2. Aliquam tincidunt mauris eu risus.
  3. Vestibulum auctor dapibus neque.

Sample Text

Lorem ipsum dolor sit amet, consectetur adipisicing elit, sed do eiusmod tempor incididunt ut labore et dolore magna aliqua. Ut enim ad minim veniam, quis nostrud exercitation test link ullamco laboris nisi ut aliquip ex ea commodo consequat.

Definition List

Definition list
Consectetur adipisicing elit, sed do eiusmod tempor incididunt ut labore et dolore magna aliqua.
Lorem ipsum dolor sit amet
Consectetur adipisicing elit, sed do eiusmod tempor incididunt ut labore et dolore magna aliqua.

Support

Need our help to upload or customize this blogger template? Contact me with details about the theme customization you need.

Pages