Manchester City Yasherekea Ushirikiano Wa Kimataifa Na Tecno Mobile
Watengezaji wakubwa wa simu za mkononi TECNO Mobile na Klabu ya ligi ya Uingereza, Manchester City leo wanasherehea uzinduzi wa ushirikiano wa kimataifa kwa miaka kadha.
Kama mshirika rasmi wa Klabu ya mpira ya Manchester City, TECNO Mobile itashirikiana na klabu hiyo kukuza mikakati ya masoko na matangazo ya kampeni sehemu mbalimbali duniani, ikiwemo bara la Afrika ambapo TECNO tayari inatambulika kama kinara wa soko la simu za mkononi.
TECNO ambayo ni sehemu ya Transsion Holdings, kwa mara ya kwanza ilianzishwa nchini China na kwa miaka kumi iliyopita imekuza umaarufu wake katika masoko tofauti zaidi ya 40 yanayochipukia ambako mashabiki wa Manchester City wapo na wanaendelea kuongezeka kila siku.
Akizungumza kwenye uzinduzi wa ushirikiano huo wa kimataifa uliofanyika kwenye kituo cha mafunzo na uangalizi wa maendeleo ya vijana, Afisa Mkuu wa Biashara wa City Football Group Tom Glick alisema “Tunafurahi kuwakaribisha TECNO Mobile katika mkusanyiko wa ushirikiano wa kimataifa, kujikita kwake zaidi katika masoko ya nyumbani kunaendana na namna ambavyo tunafanya shughuli zetu na tunatazamia kushirikiana nao kuungana na mashabiki wa Manchester City duniani kote.
Stephen Ha Mkurugenzi Mtendaji wa TECNO Mobile akizungumza katika uzinduzi katika kituo cha mafunzo na uangalizi wa maendeleo ya vijana cha Manchester City aliongezea:
“Tunashukuru sana kushirikiana na klabu yenye mafanikio na inayojulikana ya Manchester City, tutaendeleza uhusiano wetu wa muda mrefu katika michezo kwa hali ya juu”
“Kwa kuwapatia wateja wetu uzoefu wa kufurahia zaidi simu bora isiyolinganishwa na nyingine ni kipaumbele cha juu kwa TECNO Mobile na tunaona ulinganifu mwingi mno na Manchester City tukiangalia mkazo wao wanaoweka katika kuwapatia mashabiki wake uwezo wa kufurahia utofauti wa kipekee kwa njia ya mtandao.
“Tunafuraha kujiunga na timu yao na tunasubiri kwa hamu kuanzisha ushirika huu pamoja."
No comments:
Post a Comment