Trump amteua Jenarali James Mattis kuwa waziri wa ulinzi
Rais Mteule wa Marekani Donald Trump amefanya mkutano wa kwanza wa hadhara tangu kushinda urais ambapo amemtangaza jenerali mstaafu James Mattis kama waziri mpya wa ulinzi.
Jenerali Mattis maarufu kama 'Mad Dog', ni mwanajeshi wa zamani aliye na sifa ya kuweka mikakati, kuwa na msimamo mkali na mpinzani mkubwa wa Iran.
Trump alimfananisha James Mattis na Jenerali George Patton, kamanda wa jeshi la Marekani kwenye vita vikuu vya pili ambapo wenzake walimpa jina la '' Old Blood-and-Guts" kutokana na ujasiri wake.
Akihutubia mkutano wa hadhara katika jimbo la Ohio, Trump ameapa kutumia mamlaka yake kukandamiza kabisa ugaidi ndani ya Marekani.
Amesema watu wasiojulikana wanaingia Marekani kutoka Mashariki ya kati na kusema atawazima kabisa.
Rais huyo mteule amesisitiza kauli yake kwenye kampeini ya kuweka maslahi ya Marekani mbele akisema raia wa Marekani wanajali zaidi masuala ya ndani ya nchi na siyo matukio ya kimataifa.
Aidha amelaani lugha ya uchochezi na mgawanyiko.
No comments:
Post a Comment