CCM Wampongeza Mbunge wao wa CCM aliyekodi ndege Ya Kumsafirisha Tundu Lissu
Chama Cha Mapinduzi (CCM) kimempongeza mwanachama wake aliyejitolea kudhamini ndege iliyomsafirisha Mbunge wa Jimbo la Singida Mashariki, Tundu Lissu kwenda jijini Nairobi nchini Kenya kwaajili ya matibabu.
Katika taarifa hiyo, imesema kuwa wamechukua hatua hiyo ya kumpongeza Mbunge wa Jimbo la Mpendae, Salim Hassan Turky kwa kuonyesha upendo, utu na mshikamano na kuweka kando tofauti za kisiasa.
“Kwa dhati kabisa tunampongeza mwanachama wetu na mbunge wa Jimbo la Mpendae, kwa kuonyesha utu na kuweka kando itikadi za kivyama kumsaidia Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu,” amesema Polepole kupitia taarifa hiyo
Hata hivyo, Polepole ameongeza kuwa wameamua kumpongeza mbunge huyo kwa kuonyesha uzalendo wa hali ya juu, kwani katika matatizo ni vyema itikadi za kisiasa zikawekwa pembeni ili kuweza kutatua kile ambacho kinakuwa kinawakabili.
No comments:
Post a Comment