Hussein Bashe: Amani Imepoteza, Hakuna Aliye na Uhakika na Maisha Yake

Hussein Bashe: Amani Imepoteza, Hakuna Aliye na Uhakika na Maisha Yake

Mbunge wa Nzega Mjini Hussein Bashe amefunguka na kuomba muongozo wa Spika kuhusu hali ya usalama wa nchi, kwa kuwa matukio ambayo yanaendelea kutokea ya kihalifu hayana hitimisho yake.

Bashe amesema hayo wakati akiomba muongozo ndani ya bunge kwa kumtaka Spika wa bunge Job Ndugai kukubali ombi la kamati ya usalama ya bunge likutane na vyombo vya usalama ili yaweze kupatikana majibu ya matukio yanayoendelea kutokea.

"Mhe. Spika katika taifa letu katika kipindi cha muda mrefu kumekuwa yakitokea matukio mbalimbali ambayo sisi kama wawakilishi wa wananchi tuna wajibu wa kupata taarifa sahihi juu ya muendelezo wa matukio hayo ambayo hayana hitimisho", amesema Bashe.

Pamoja na hayo, Bashe aliendelea kwa kusema "sisi tunawawakilisha Watanzania milioni 50 lakini matukio haya yanayotokea yanaharibu heshima ya taifa letu ningekuomba kama utaridhia na wabunge wataniunga mkono, uitake kamati yako ya ulinzi na usalama ya bunge tukufu ikutane na vyombo vya ulinzi na usalama ili tuweze kupata taarifa kamili juu ya mambo haya yanayoendelea katika taifa letu, ili Watanzania na sisi wabunge tuwe na uhakika kwa sababu hali inavyoendelea hakuna mtu mwenye uhakika na maisha yake ya kesho. Dhamana tuliyopewa sisi dhamana ya kusimamia mali, usalama pamoja na raia wa nchi hii", amesisitiza Bashe.

Kwa upande wake Spika wa Bunge Mhe. Job Ndugai alikubali hoja iliyotolewa na mbunge Bashe na kutoa amri  kwa kamati ya ulinzi na usalama ya bunge iende kukutana ili wapange ni jinsi gani ya kulishughulikia jambo hilo na watakapokuwa tayari kabla bunge kuhairishwa siku ya Ijumaa wiki ijayo warudishe majibu kwa bunge juu ya walichoamua.

Share:

No comments:

Post a Comment

Categories

Ordered List

  1. Lorem ipsum dolor sit amet, consectetuer adipiscing elit.
  2. Aliquam tincidunt mauris eu risus.
  3. Vestibulum auctor dapibus neque.

Sample Text

Lorem ipsum dolor sit amet, consectetur adipisicing elit, sed do eiusmod tempor incididunt ut labore et dolore magna aliqua. Ut enim ad minim veniam, quis nostrud exercitation test link ullamco laboris nisi ut aliquip ex ea commodo consequat.

Definition List

Definition list
Consectetur adipisicing elit, sed do eiusmod tempor incididunt ut labore et dolore magna aliqua.
Lorem ipsum dolor sit amet
Consectetur adipisicing elit, sed do eiusmod tempor incididunt ut labore et dolore magna aliqua.

Support

Need our help to upload or customize this blogger template? Contact me with details about the theme customization you need.

Pages